NEW STORY: "DE LIFE I DESERVE" PART ONE

Dampa

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2017
Posts
810
Reaction score
1,264
Basi bhana baada ya kuachana na mama na maneno yake ya kila siku kuhusu kutafuta kazi kuliko kushinda kwenye vilinge na masela na wana,Nikazama gheto kwangu huku nimechoka na kinjaa uzembe kikizidi kulisokota tumbo langu.Lengo halikuwa kulala wala nn ....Yalaaah ! Kumbe dg P kasepa nayo.Nilijisemea kimoyo moyo baada ya kukuta buku langu halipo juu ya meza .Itakuwa dg P tu kaondoka nalo.Mama yangu hapo ndo njaa ikawa kama imetiwa ndimu na pilipili mpaka nikajikuta najuta kwanini asubuhi nilimchenga mshua aliponipa deal ya kuosha gari yake.
Lakini sio kesi sababu hata mimi huwa namchapa sana dg vibuku buku vyake wakati sina nauli ya kwendea town kwenye amshaamsha zangu.Dogo langu nampenda sana tunaishi km tupo mbele kwa love tunayooneshana. Ni mcheshi,mpole ,hardworking na hapendi mambo ya kijinga jinga yani kum-face inabidi ujipange lasivyo atakuaibisha cz he is a good thinker. Ni mdogo Kiumri (14) lakini ana busara kama mtu mzima japo yupo darasa la 5.
Wakati nikiwaza na kupotezwa katika wimbi la mawazo lilochanganyika na kinjaa flan hv amaizing,Ilikuwa yapata kama saa saba kasoro hv nilishitushwa na mlio wa simu yangu kuashiria kuna ujumbe umeingia.Aagh nikaupuuzia nikijua ni voda tu hao wananidai wananikumbusha deni lao cz inakaribia kukata mwezi sasa sijaweka vocha toka nikope.Zaidi anayeniokoa ni demu wangu wa chuo ambaye huniungia kifurushi pale asiniona online.
Oooooh men wtf ! ,sema kibishi tu mzee bhabha nakomaa.Heee ! Eeeh ndo hivyo usawa wenyewe ndo kama huu basi nikaichukua simu kizembe zembe toka kwenye charge kisha nikajibwaga kitandani huku nashauku ya kujua ujumbe unasema vp.Lakini kabla sijafungua nikasikia maza ananiita kwa sauti ya juu na ya ukali,in short mim na bi mkubwa huwa tunapelekana kibabe sana kiupande wake hanikubali sana kama anavyonikubali mshua so most of the time tunalumbana hapa na pale but all in all tunapendana sana.
Nadhani sijui ni tabia yangu kutopenda kuingiliwa kwenye maamuzi yangu especially Mwanamke ndo kitu ambacho tunalumbana sana na bi mkubwa si kwamba namdharau lakini ni kitu ambacho kiko ndani yangu hata yeye analijua hilo.Mara kadhaa huwa anasema nina tabia kama za baba yake ambaye ni babu yangu,basi mimi huishia kucheka tu ndo hapo anafura tu kisha namtania kwann Mama yake aliweza kuishi na babu yeye atashindwa vp kama ni hivyo mama hubaki anatabasamu halfu nammaliza kwa kumwambia aniite baba.In short Family yetu tunapendana sana najivunia kwa hilo aiiise.
Basi bwana Ghafla nikaibuliwa kwenye lindi hilo na makelele ya mama huku anagonga mlango kwa nguvu sana mpaka nikapatwa na hofu.Wakati mwanzo anaanza kugonga nilichukulia kawaida tu sababu nilisha mzoea mama gonga yake ni ya fujo anaponihitaji nikiwa gheto lakini leo alinitia hofu sana cz siyo kawaida..
Kwa kasi ya ajabu nikasimama nakushika funguo cz ninapoingia gheto mm lazima nitie funguo kabisa.Ghafla nikaminya kitasa mlango ukafunguka,nikapigwa butwaa nilichokiona mbele ya macho yangu sikuamini..........!!!

Je nn nilikiona fuatana nami next time usisahau kushare kukoment na kutukana pia unaruhusiwa ila siyo ya nguoni.....Natania
Tchaooooo.!!!?
By Dampa
 
Pamoja mkuu

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Upuuzi wskukatisha story ........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…