NEW WORLD BANK MANAGING DIRECTOR Okonjo-Iweala IS A NIGERIAN

Nigeria settles Paris Club debt






Soma hapa

Kwa hiyo madeni siyo yalifutwa bali waliweza kupunguziwa riba na kulipa deni.
 
mbona Dr.Basil Mramba amefanya kazi kubwa tu. Ameteremsha inflation, amewezesha kufutiwa madeni, etc etc. Mbona sijasikia akipewa sifa kama za Dr.Ngozi?
 
Dua,Shukran kwa masahihisho ya post yangu iliyoeleza kuwa Nigeria "walifutiwa" Madeni yao.Ukweli wa mambo ni kwamba "walilipa" Kama inavyoonyeshwa ktk post yako.Naomba lawama zote kuhusu post hiyo zielekezwe kwangu, sioni sababu ya kumuandama Game Theory kwamba alete datas kuthibitisha ukweli wa Maandiko hayo.Niliyeandika ni Mimi na si GT.Naomba tuwiane radhi kama kuna usumbufu wowote niliyosababisha kwa kuweka post hiyo!,na tuendelee kusahihishana popote panapoonekana pana utata.
 



Mwawado nashukuru kwa kuja. Mimi kusema ukweli nililiona hilo lakini sikutaka kubishana na magazeti na nikatoa source ambayo ina info zote kuhusu Nigeria kule WB

Once again nakupa respect kwa kuja na kuweka mamabo sawa

Much props bro
 
Huyu mama kiboko, CV yake imenihehusha; pia amesoma vyuo vyenye akili vyote. Kwa kweli bi kudos kwake sana tu na kwa wanawake wa bara hili pia. Safi sana!
 

Mwawado nashukuru kwa kuja. Mimi kusema ukweli nililiona hilo lakini sikutaka kubishana na magazeti na nikatoa source ambayo ina info zote kuhusu Nigeria kule WB

Once again nakupa respect kwa kuja na kuweka mamabo sawa

Much props bro

Hukuona lolote u-pimbi wako tu. Kazi ku-paste malink bomu.
 
wenzetu Nigeria inaonekana wana benefit from high oil prices,jee sisi vipi na gold yetu ambayo price sasa is almost all time high...ni nimeona one requirement ni all foreign companies lazima waonyeshe how much they pay the government (publicly) nafikiri hii ni nzuri tukicopy ili tujue Buzwagi,Kempisk,Geita etc wanatulipa nini kila mwaka sio nyimbo tuu za uwekezaji
 
Hukuona lolote u-pimbi wako tu. Kazi ku-past malink bomu.

Mkuu Dua,

Heshima mbele mkuu, hii ni below the belt mkuu wewe na mkuu Theory, ni wachambuzi wakali sana hapa forum, na mnaheshimika sana, na binafsi siielewi vizuri hiii topic ndio maana sijaichangia,

lakini nilipoiona nilidhani na bado ninaamini kuwa ni topic bomba sana na kwamba Theory, amejitahidi sana ku-paste huko na kutuletea hapa forum, maana tusingemjua huyu mama vizuri,

Kwa hiyo mkuu kwa maoni yangu, hapo umechezea rafu mkuu Theory, yaani below the belt, unless kuna something sijui! tukubali kutokubaliana kama Zitto na Karamagi, lakini tuendelee kuheshimiana wakuuu!
 
Game Theory

ha ha ha haaaaa haaaaaaaaaaaaaa...............................Mimi nilifikiri ungeweka picha ya pimbi kumbe umeweka picha yako nini?
 



Heshima mbele Mkuu

Ukisoma vizuri kuanzia mwanzo utaelewa jinsi majibu ya kifedhuli yanavyoweza kujibiwa hapa (kumkoma nyani giladi). Hoja hujibiwa kwa hoja kama Mzee Mwanakijiji anavyosema kila wakati. Lakini hoja nzito kama hii ikikushinda na baadaye ikidhihirika usianze kutoa baseless lawama na kuikejeli JF ambayo umeingia kwa hiari yako mwenyewe. Tupo hapa kutetea maslahi ya WTZ wengi ambao wengine hawana uwezo huo na Mafisadi wanataka kutumia kila mwanya kupindisha hoja za msingi ambazo zinawekwa hapa kila uchwao.

Sidhani kama kuna JF member hapa ambaye yeye ni gazeti? Au kuna mwana forum yoyote ambaye mawazo yake hayahitajiki, kila wazo ni la muhimu na wazo lolote linawakilisha WTZ wengi ambao hawaandiki. Hakuna sababu ya kukejeli JF na members wote bila sababu zozote za msingi. NATUMAINI UMENIELEWA THANKS.

Tuendelee kumkoma huyu nyani kabla hajaanza kupanda kwenye miti.
 
Kitila Mkumbo said:
Huyu mama kiboko, CV yake imenihehusha; pia amesoma vyuo vyenye akili vyote.

Kitila,
Waswahili wana msemo wao ati ngombe wa maskini hazai. Tanzania tulipata kuwa na waziri wa fedha,Dr.Malima, mwenye elimu kama ya huyo Mama, lakini sisi tukaishia kufungiwa misaada na wafadhili.

Dr.Kighoma Ali Malima alisoma BA.Econ Williams & Mary, Masters akachukua Yale, na PhD akapata toka Princeton.

Mwawado said:
Mama huyo ni Member kwenye MO-Ibrahim Foundation na US Federal Reserve.

Mwawado,
Maelezo yako kuhusu Dr.Ngozi na US Federal Reserve sijayaelewa kidogo. Je, ulimaanisha member wa board of governors of US Federal Reserve?

Nafasi hiyo naamini mhusika hupendekezwa na Raisi wa USA na kuthibitishwa na Senate. Board members wa US Fed Reserve huteuliwa kutumikia kipindi cha miaka 14??!

Sasa ukiangalia hiyo ni nafasi NYETI na NZITO kwelikweli ktk sekta ya fedha ya USA. Ikitakuwa vizuri kama ukitupatia ufafanuzi na maelezo ya ziada ktk suala hili.
 
Mwawado,
Maelezo yako kuhusu Dr.Ngozi na US Federal Reserve sijayaelewa kidogo. Je, ulimaanisha member wa board of governors of US Federal Reserve?

Nafasi hiyo naamini mhusika hupendekezwa na Raisi wa USA na kuthibitishwa na Senate. Board members wa US Fed Reserve huteuliwa kutumikia kipindi cha miaka 14??!

Sasa ukiangalia hiyo ni nafasi NYETI na NZITO kwelikweli ktk sekta ya fedha ya USA. Ikitakuwa vizuri kama ukitupatia ufafanuzi na maelezo ya ziada ktk suala hili.[/QUOTE]

*************************************************************************************

Kaka Joka kuu,Ni kweli kwamba Governors wa Fed Reserve ni nafasi nyeti na Muhimu kwenye Taasisi ya pesa USA.Na kwa sheria za Fed nafasi hizo huwa kwa Wamarekani 7 na huwa hapo kwa muda wa miaka 14 baada ya kuthibitishwa na Senate,hivi sasa 2007 wapo (Board Members),Governors 5 wakiongozwa na Ben.S Bernanke.

Kwa ufahamu wangu Mama Ngozi alikuwa ktk Board hiyo kitengo kinachoitwa FOMC (Federal Open Market committee),alikuwa anaingia kwenye Board hiyo kama Mkuu wa kitengo kilichoitwa Globalization,Macroeconomic performance & Monetary Policy,hakuingia humo kama Governor au Bank President bali alikuwa Mkuu wa kitengo.Kuwa ktk Board ya FOMC hakuhitaji Uthibitisho wa Senate.(Pitia Muundo wa Federal Reserve)

Katika FOMC pia kulikuwa na Waafghani wawili ambao ni Prof.Anwar na Dr.Ashraf Ghani ambao wote kwa wakati tofauti wamewahi kufanya kazi World Bank.
 


MWAWADO

sina la zaidi


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…