Watu kama kina Kiranga ukiwaambia hivyo watakuelewa?
Afadhali New York nimeishi, napajua, kuna wenzangu wanapajua, kwa hiyo najua pana exist na nikitaka kurudi kuhakikisha bado papo intact.
Huko mbinguni kuna mtu kashafika? Unaweza kutupa ushahidi gani zaidi ya mapokeo ya kidini kuthibitisha kwamba kupo?
Na kuhusu New Yorkers kuonyesha sehemu nzuri tu, wao hawajasema kwamba New York yote iko hivyo.Hata sisi tukitaka kuitangaza nchi yetu tunapiga picha sehemu zinazovutia tu, hatupigi picha Manzese Uwanja wa Fisi na kwa Mfuga Mbwa .Ukitaka kuonyesha ubaya wa New York kapige hizo picha, au zitafute online utuonyeshe.
Hata Nyerere aliwaasa msiangalie mabaya yake tu bila kuangalia mazuri.Hata kama unataka kusema unataka kuwa balanced, on the whole, mazuri ya New York yana outweight mabaya yake. Hizo projects mnazozisma nyingine nzuri kuliko Upanga uhindini, na zaidi ya hayo hazikatiki umeme wala maji. Watu wana parks and recreational facilities ambazo hata Oysterbay yetu haina, sembuse huko Manzese kwa Mfuga Mbwa Uwanja wa fisi.
Kwa hiyo stop with the negativity already, kama wenzetu wana cover negative side ya Africa tu, hawaonyeshi sehemu nzuri, that is wrong and we should point that out. But that does not mean we should do the same thing and dwell on their bad side.Tutakosa moral authority ya kuwasema. Again, for the umpteenth time, two wrongs do not make a right.