Newcastle United 0-1 Manchester City: Pep hashikiki, afikisha mechi 20 bila kupoteza

City tangu lini ilikuwa mbovu? Labda City ya Enzi hizo ila tangu wapate pesa City haijawahi kuwa mbovu na always huwa ina kikosi kipana, money talks
 
City tangu lini ilikuwa mbovu? Labda City ya Enzi hizo ila tangu wapate pesa City haijawahi kuwa mbovu na always huwa ina kikosi kipana, money talks
City ilikuwa mbovu ukilinganisha na city hii ya pep?.

City ipi iliwahi shinda mechi zaid ya 10 bila kupoteza mchezo?.
 
City ilikuwa mbovu ukilinganisha na city hii ya pep.

City ipi iliwahi shinda mechi zaid ya 10 bila kupoteza mchezo?.
Hapa sipingani na record, ila napingana na hoja kuwa alikuta City mbovu wakati ni timu hiyo hiyo ambayo ilikuwa imeweka rekodi kwa Mara ya kwanza kufika mbali kwenye UEFA chini ya pellegrini, unaposema ilikuwa mbovu kisa rekodi basi hata mtu akija Leo na hoja kuwa Harry Kane msimu uliopita alikuwa mbovu kisa rekodi aliyoweka mwaka huu ni tofauti na mwaka uliopita tutashindwa kumpinga hali ya kuwa the man was top scorer. Lazima tukubali kuwa Pep ameleta impact kubwa msimu huu ila City haijawahi kuwa mbovu Kwa miaka ya hivi karibuni
 
Mkuu kinachoangaliwa hapa nafikiri ni impact kubwa ameyoleta Pep msimu huu.Pep wamsimu uliopita ingawa timu yake ilishika no 3 lkn watu walimbeza kwakuona kuwa kafeli.

Pep msimu huu kadrop wachezaji nane, lakini amefanya vizuri zaid yawatu walivyotarajia.

Sikumbuki nilini kabla ya January gap lilikuwa point 15 kati ya timu yakwanza na yapili.

Man city hii ya sasa nitofauti na Man city yeyote ile iliyowahi kuwepo,kuanzia uchezaji namna wanavyocheza.

Tunachojiupiza sisi wengine iweje timu kama man city ambayo ukilinganisha na PSG bado inaonekana yakawaida iongoze point 15 kwenye ligi bora duniani,ambayo watu wanadai inaushindani mkubwa?,ukilinganisha na ligi nyingine duniani?.

Je ligi ya EPL nikweli nibora ukilinganisha na Laliga?.

Au EPL niligi maarufu tu usiyo na ubora.
 
Zama hubadilika mkuu, hebu jaribu kuangalia hata ubora wa timu za EPL msimu huu, timu nyingi hazina consistency, jaribu kuangalia hata idadi ya makocha walio timuliwa mapema msimu huu, Tusisahau hata Leicester ilikuwa tishio sana msimu ule ilipochukua ubingwa, Pep yuko vizuri na mbinu zake Kwa msimu huu zinafanya kazi, so tuendelee kuenjoy mpira, ila ubora wa City usitufanye tudharau timu zingine, kupitia Pep nadhan other managers watajifunza kitu na Kuja na mbinu mpya na hapo ndipo tutaona utamu wa EPL ukinoga zaidi
 
Asante mkuu naunga mkono hoja yako hapa.
 
ananunua wingbacks kwa bei ya striker
 
Anaweza akaweka record ambayo itakuwa ngumu sana kufunjwa katika kizazi hiki cha mpira wa miguu
Kweli ukiangalia ana mechi mbili zijazo ni lain (crystal Palace na Watford) kabla ya kucheza na Liverpool. Obvious anaenda kushinda mechi 20 mfululozo kitu ambacho ni kuziaibisha timu za uingereza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…