News alert: Makamu wa rais chuo kikuu tumaini dar kuburuzwa mahakamani.

Sir-mganah

Member
Joined
Jul 17, 2011
Posts
58
Reaction score
11
Ndugu wana jf taarifa tulizozipata hivi punde ni kwamba ndg: JACKSON SHUMBI aliyekuwa makamu wa rais na anayemaliza muda wake kwa nafasi hiyo amefunguliwa mashtaka katika MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kwa kile kinachodaiwa kuwa alishirikiana na management ya chuo hicho kubatilisha matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi mpinzani wake kama ilivyotangazwa na tume ya uchaguzi chuoni hapo mapema mwezi may.
Habari za kina zinasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa umegubikwa na wingu zito la dhuluma na michezo michafu na kwamba mgombea aliyetangazwa mshindi hakushinda kwa halali kutokana na kuwepo kwa ukweli kwamba alidiriki kughushi vitambulisho vya wanachuo na kuwaingiza watu ambao hawakuwa wanafunzi wa chuo hicho ili kumpigia kura kitu ambacho baadaye kilithibitishwa na jeshi la polis
Akithibisha kuwepo kwa njama hizo mmja wa askari kanzu kituo cha polisi cha chang'ombe alithibitisha kukamatwa kwa mabinti wawili ambao ni mama ntilie maeneo ya kurasini waliokiri kupewa kadi bandia kisha kujifanya wanafunzi wa chuo hicho na ksha kupiga kura.
kesi hiyo ianatarajiwa kuanza kusikilizwa august mosi katika mahakama kuu ya Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…