Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 55
Mojawapo ya kazi ya Rais ni kuteua wasaidizi wake watakaomsaidia
kuongoza wizara kadhaa alizoziunda. Kama ambavyo Kasheshe
ametangulia kusema kwamba mawaziri ni wasimamiaji wa utekelezaji
wa sera za chama kilicho madarakani, mimi napenda kuongezea kwa
kurudia kuwakumbusha wana-JF kuwa uendeshaji wa shughuli za
wizara hufanywa na technical people wakiongozwa au kusimamiwa na
katibu mkuu wa wizara husika. Kwahiyo uteuzi wa mawaziri wa
kumsaidia Rais sidhani kama nina haja ya kuhoji ilhali mwenye
kuwateua wamsaidie hana tatizo nao. Ni vema tukakumbuka kuwa
Rais wa Tanzania ni mmoja tu.
I have no objection kwa wote walioteuliwa.
1
According to the dataz, huyu mkulu ni ndugu wa karibu wa muungwana, level ya ujomba, uwezo wake kikazi haufahamiki ila ni mstaarabu na ni mkimya huwa haongei kabisa! Sasa tutaaamua wenyewe kama anafaa, au?
2.
According to more dataz, huyu mkulu alikubali kutumiwa na Lowassa kutaka kuuvuruga mkutano wa NEC kule Butiama, akaomba kusema, na kuanza kudai kuwa kwa nini Lowassa hakupewa nafasi ya kujitetea, akaambiwa kwa lugha ya ukali sana na muungwana, kuwa akae chini na anyamaze, kwa hii ilikuwa ni kifuta jasho!
Ukimweka prof. wa mifugo hapo, kuna kazi kweli mpaka aje aelewe dunia ya mawasiliano inaenda wapi.
Prof. Mwandosya alikuwa na mwelekeo mzuri kwenye hiyo wizara, ila tu wizara yake ilikuwa kubwa mno na hivyo kumezwa na miundo mbinu ambako kuna matatizo kila siku.
Kosa kubwa tunalofanya Watanzania na hata hapa JF ni kufikiri ubora wa kiongozi unatokana na kupiga kwake kelele bungeni au sehemu yoyote nyingine.
Ubora wa kiongozi unatokana na uwezo wake wa ku deliver na upimwe kwa mafanikio yake kwa kazi za nyuma.
Mtu anayeshindwa ku deliver kama mbunge sidhani kama ataweza kufanya hivyo kama waziri au kama rais.
Ni rahisi mno kuwa mpinzani au kuwa backbencher na kukosoa kila siku kama tunavyofanya hapa JF lakini ni kitu kingine kupewa usukani na kuambiwa sasa
lisukume hili gari letu kwenda kwenye nchi ya maziwa yanayotoka kwenye bomba.
Usomi ndio una faida lakini ni kigezo cha chini kabisa, ni indicator moja tu kati ya nyingi ambayo inakufanya uingie kwenye 100 bora kama lengo ni kumtafuta mtu mmoja.
Kwa dunia ya leo mtu yeyeote mwenye degree moja anaweza kabisa kuwa waziri mzuri sana ili mradi awe na sifa hizo zingine.
Tumeona maprofesa wetu wanavyochemsha kwenye wizara, tumeona madkatri ambao
hata hawafai kusimamia nyumba zao.
Hawa mawaziri wote ni wabunge, ingefaa tunapowajadili, basi tuanze na je kule wanakotoka wamefanya nini? Kama mtu anashinda kuzunguka Dar na Dodoma na kuacha jimbo lake linadumaa, mnafikiri akiwa waziri au rais kwanini asiwe naye Vasco Dagama? Wote tumeona ya JK, kila mtu alidhani ataleta maajabu, laiti tungejiuliza mapema, je kafanya nini kule kwenye jimbo lake? Huenda wala tusingeliweka matagemeo makubwa.
Mojawapo ya kazi ya Rais ni kuteua wasaidizi wake watakaomsaidia
kuongoza wizara kadhaa alizoziunda. Kama ambavyo Kasheshe
ametangulia kusema kwamba mawaziri ni wasimamiaji wa utekelezaji
wa sera za chama kilicho madarakani, mimi napenda kuongezea kwa
kurudia kuwakumbusha wana-JF kuwa uendeshaji wa shughuli za
wizara hufanywa na technical people wakiongozwa au kusimamiwa na
katibu mkuu wa wizara husika. Kwahiyo uteuzi wa mawaziri wa
kumsaidia Rais sidhani kama nina haja ya kuhoji ilhali mwenye
kuwateua wamsaidie hana tatizo nao. Ni vema tukakumbuka kuwa
Rais wa Tanzania ni mmoja tu.
I have no objection kwa wote walioteuliwa.
Jamaa kweli kachoka, naona kabisa si muda tena atabadili baraza, na ndio utakuwa mwisho wake, maana hatutaendelea kunyamazia kubadili wezi wakati sisi huku tunakufa njaa
Mwanri pia ni mzalendo sana, ni chaguo zuri ingawa angefaa kuwa Waziri Kamili. Jamaa ni marxist huyu, acha!
Kuhani Mkuu,
Na huu ni ndio upumbavu na uhuni watanzania tunaoupigia makelele... ati tunafikiri billioni moja(1) ya mzee wa vijisenti itaondoa tatizo la uchumi.
Siku moja nikakutana na mkaanga Samaki pale Dar es Salaam akaniuliza hivi, "Hivi kaka hizo fedha za EPA zikirudishwa mambo yatabadilika eeeh" nikamwambia sio fedha za EPA tu, na Za Meremeta n.k. ni maji ya kifuu kwenye bahari... ni kitu kidogo sana kwa uchumi wa nchi... tufanye kazi ndio njia ya kukomboa taifa.
Lingine ni Ujinga pia kudhani kwamba Rais alitakiwa kufanya mabadiliko makubwa kipindi hiki ambacho baraza lina miezi michache sana.
Kibaya zaidi vyama vyetu makini wakombozi wa wananachi wanafanya kwamba hizo ndio hoja kuu za kufanya uchumi ukue!!! Taifa linazama hili chini ya CCM au hata chini ya Kile chama makini.
Kwanza:
Ilikuwa ni Jambo jemaa kutoleta waziri mwingine mpya... kwanza kama habari ziko kamili kweli, atakuwa ampenguza waziri mmoja, kwenye baraza lake.
Pili:
Wizara ya Miundo Mbinu ni wizara nyeti sana, fedha nyingi zinaenda huko kupeleka mwadilifu na huenda mtu anayemwamini ni njia moja ya kulinda masilahi yetu wananchi.
Tatu:
Tusichanganye mambo mawaziri ni wanasiasa, kazi ya msingi inafanywa na makatibu wakuu na wakurugenz;
Nne;
Waziri ni mtizama masilahi ya wananchi akipenda of course maana anaweza angalia masilahi yake... lakini zaidi Waziri ni mtu anayeangalia kwamba sera za chama chake kama zinatekelezwa vizuri.
Jamani Magufuli Pombe kapelekwa wapi? Au ndio kazimwa? Au yuko katika kashfa zinazokuja za EPA au za nyumba?
Mzalendo gani mwizi tu huyo? Waulize wakazi wa siha wakueleze ukweli. Mwanri ni mwanachama halisi wa Chama Cha Mafisadi, unajua kwani nini uliondolewa kwenye uenezi CCM?
Marxist gani? Huyu naye ni bepari uchwara. Ni wanafiki wenye kujifunika kwa kivuli cha marxism kama alivyokuwa Kingunge Ngombare Mwizi.
http://www.chadema.net/makala/kafulila/david_6.html
Umesahau haya makala?
http://www.chadema.net/makala/kafulila/david_6.html
Halafu unakumbuka kauli ya Mwanri alivyokuja kwetu Zanzibar?
Asha
kwi kwi kwi... Zitto Nyang'anya kadi hii mwanachama yako... haiheshimu yeye kwamba iko kaa na Mwanri kwa miaka miwili... sheee, napandishi mori shikilia mimi!!! hii ndio torono tukulu!!!
Torono -- maana yake "mtukukutu" kwa kimasa
Tukulu ---maana yake "saba" jwa kimasai
kwi kwi kwi... Zitto Nyang'anya kadi hii mwanachama yako... haiheshimu yeye kwamba iko kaa na Mwanri kwa miaka miwili... sheee, napandishi mori shikilia mimi!!! hii ndio torono tukulu!!!
Torono -- maana yake "mtukukutu" kwa kimasa
Tukulu ---maana yake "saba" jwa kimasai