[news alert] waliochaguliwa ardhi university 2013/14

Jerhy

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2013
Posts
3,134
Reaction score
998
Tunayo pongezi kubwa kwa vijana wote waliochaguliwa kujiunga na chuo kikuu Ardhi kwa mwaka wa masomo 2013/14. Chuo kipo jijini Dar es Salaam karibu na UDSM.

Nianze kwa kukufahamisha jinsi ya kufika hapa, kwa wale watakaotoka mikoani , ukishuka tu ubungo kituo kikuu cha mabasi, toka nje uliza Sam Nujoma Road hii inanzia pale ubungo mataa kuelekea Mwenge hivo basi daladala za kwenda chuo zinapatikana pale darajani njia panda ya chuo kikuu, zimeandikwa Mwenge-Ubungo via Chuo kikuu nauli ni shilingi 400/= tu. Usikodi taksi 15,000/= hiyo utaijutia kwa sababu hapa hakuna atayekupokea ni wewe na begi lako kwani hata siku hiyo hutaonyeshwa mahali pa kulala hivo ni kuripoti na kusepa . Mpaka utakapo kamilisha malipo yote. Kwa hiyo Utashukia Ardhi au Geti dogo hapo utakuwa umefika Ardhi Univesity.

Mambo muhimu ya kuzingatia ni haya:
1. Chuo kina hostel ya waschana na wavulana yenye uwezo wa kubeba wanachuo 400 tu kila mwaka. Hivo ukiwahi kuripoti na kulipia pango basi ndo bahati yako pekee ambapo gharama zake ni120,000/= kwa semester per head. Ukikosa hosteli hiyo ipo nyingine nje ya chuo mitaa ya Lufungila ambayo gharama yake iko juu kidogo. Kwa hiyo njoo na fedha ya kutosha kuweza kujikimu.
2. Tuliowengi tumepanga mtaani survey na mlalakuwa huko vyumba ni kuanzia 60,000/= na kuendelea.
Hivyo basi jitahidini kuweka uhusiano mzuri kwenu wenye ndugu, jamaa na marafiki waliopo dar ili waweze kukuhifadhi kwa muda wakati ukisubiria mkopo loan bodi na kulipia pango.
3. Hakikisha unahudhuria orintation course kwa uaminifu zaidi kwani meng kuhusu mfumo mzima wa jinsi utakavyoishi hapo chuo hutolewa kwnye mhadhara huo, pia jitahidi kupsa ratiba ya matukio kutoka kwa mshauri wa wanafunzi.
4. Chuo hiki kinakazia zaidi elimu hivo wale wanaofikiria eti wiki ya kwanza hamna kitu sio kweli, ratiba inaheshimiwa zaidi kuliko wewe yaani profesa anaingia dakika tano kabla ya muda, anatoa logistic sheet ya kusaini mahudhurio baada ya dakika 15 kupita anaichukua kisha wale watakaofika kwa kuchelewa ni kwamba haeakuhudhuria lecture zake. Hawajali mpo 3 au 7 siku hiyo yeye atafundisha mada husika, na kutoa asgnment. Hivo mahudhurio yako mazuri ndo yatakuepusha na kurudia mitihani na diskondinuesheni.

5. Vifaa vya darasani katika fani za uchoraji vinapatikana katika stationary zetu chuo kwa bei nafuu zaidi.

Mwisho tunakukaribisha sana chuo kikuu Ardhi tarehe 14/10/2013
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…