Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
With all due respectaombe radhi kwa lipi? kwa kuongea anachokifikiria kuwa ni sawa?
Hana haja ya kuomba radhi,tena mimi naunga mkono kabisa ,hilo ni wazo lake binafsi na sababu zipo wazi wala huna haja ya kufikiria kwa nini,hata wanyama aina ya ng'ombe mbuzi nao huwekwa alama ili kuwajua na kuweza kuwabagua kirahisi wanapoingia katika mkanganyiko.
Na hawa waathirika ikiwa watapatiwa alama flani basi watafahamika na mwisho watazoeleka na wao kuzoea hali hiyo,mboni kuna wengine wanajijulisha na wana andaa makongamano makubwa makubwa na wengine huvaa na beji kabisa ili kuwajulisha na kuwatahadharisha wengine,sasa hawa ikiwa watakubali kwa ridhaa yao wataipatia jina Tanzania katika kilingo cha Kimataifa na naamini kabisa nchi nyengine zinaweza kuiga mfano wa wagonjwa wa kwetu au mpaka waseme wazungu kama mikataba ni mibaya.
Inawezekana ana mtindio wa Ubongo....mimi nashauri kabla ya kushurutishwa kuomba radhi apimwe akili
mwiba anayo haja ya kuomba radhi kwa unyanyapaa aliyoonyesha kama binadamu. Hivi kweli unaweza toa mfano wa ng;ombe na binadamu???? haiingii akilini, sisi ni binadamu tuna haki ya kuishi huru, na tuna haki ya kupendwa hata tukiumwa.Hana haja ya kuomba radhi,tena mimi naunga mkono kabisa ,hilo ni wazo lake binafsi na sababu zipo wazi wala huna haja ya kufikiria kwa nini,hata wanyama aina ya ng'ombe mbuzi nao huwekwa alama ili kuwajua na kuweza kuwabagua kirahisi wanapoingia katika mkanganyiko.
mwiba anayo haja ya kuomba radhi kwa unyanyapaa aliyoonyesha kama binadamu. Hivi kweli unaweza toa mfano wa ng;ombe na binadamu???? haiingii akilini, sisi ni binadamu tuna haki ya kuishi huru, na tuna haki ya kupendwa hata tukiumwa.
Tuwabague ili iweje?
Kama suala ni kuwatahadharisha wengine mara ngapi tunapigiwa kelele misikitini na kanisani. Tuwe waaminifu kwenye ndoa zetu, kwa wapenzi wetu. Hilo halitoshi? Hivi tumekosa utashi kiasi gani sisi wanadamu?
Kila mtu mwenye akili timamu anajua Ukimwi unaenezwa kwa njia gani sasa kwa nini asijilinde binafsi?
Mtu akitaka kuutangazia umma kuwa ana ukimwi well and good let him do that but asifisiwe ajitangaze.
Hivi unafahamu malaria inaua kuliko ukimwi? kwa nini wasisieme basi tuwabadikie wenye malaria maana tukikaa nao au kulala nao na bahati mbaya tukang'atwa na mbu mmoja basi tushaukwaa ugonjwa sugu afrika malaria?
Embu kwanza kabla ya kuunga mkono hoja zinazohusu undani wa watu tujikague wenyewe. Nani msafi? Nani hafanyi ngono na mtu asiye mkewe/mumewe. nani hafanyi ngono kabla ya ndoa? Na wangapi hupima ukimwi kabla ya kuanza mahusiano?
tusipende kuona wengine wana matatizo wakati in reality we ourselves ndio vyanzo vya matatizo.
Yono omba radhi baba.