Ney wa Mitego anatafutwa na polisi kwa kutishia kumuua rafiki yake wa karibu

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Msanii wa Hip Hop Tanzania Emanuel "Nay wa Mitego True Boy" anatafutwa kwa kosa la kutishia kuua.
Kwa mujibu wa Suddy Baya ambae ndie alietishiwa kuuliwa na Nay, anasema kuwa amekuwa akipokea ujumbe wa vitisho mara kwa mara kutoka kwa Msanii huyo pia amekuwa akiwatumia watu tofauti tofauti ili wamteke, na kuthibitisha kwa hilo ameshapokea simu za vitisho kutoka kwa watu tofauti huku akisema walikuwa na lengo la kumteka.

Hapo mwanzo walikuwa wakiishi pamoja huku akiwa kama msaidizi wa msanii huyo katika mambo yake ya Muziki na hata huduma za nyumbani kwa maana walikuwa wanaishi nyumba moja. Mpaka anafukuzwa na Nay tayari alishafikisha miaka mitano wakiwa pamoja huku akiwa amepoteza muda wake mwingi bila mafanikio yoyote. Lakini licha ya kufukuzwa na kuondoka anasema aliendelea kufatiliwa na kupigiwa simu mara kwa mara na Nay akimuuliza maswali ambayo kwa msingi wake hayana hata maana, Moja ya swali ambalo Nay alimuuliza Suddy kama ana namba ya Mpenzi wake Siwema lakini alimjibu kuwa hana bali ana ya Dada yake Siwema ambae anaitwa Mage ndipo utata ukaanzia hapo na kumwambia afute hiyo namba na asiwasiliane na watu hao wawili, kwa mujibu wa Suddy alikubali kufanya hivyo ili kuepusha mzozo.


Suddy alisema hivi "Iko siku tukiwa na wasanii flan ivi tunakula chakula cha usiku kijitonyama nikiwa na (Climax Bibo), (Shebby Love) na (Smocka) alisema mimi na roho mbaya sana naweza muwekea sumu kwenye chakula kiukweli iliniuma nikamuona mtu wajabu sana.. Kwa kuwa mimi mdogo wake niko naye mwaka wa 5 napika miaka yote nafanya kazi zote za ndani leo hii eti nikamuweke sumu kwa kuwa ashakuwa Staa au!! Ndipo nikawa niko na hasira nikimfikria kauli yake ya mimi kumuuwa basi kuna siku akaniita mimi na dogo anaitwa dogo b.. Akatufuza tukaondoka ila dogo kupitia (Cwema aliniomba nimshawishi Dogo arudi kwa Nay ila mimi nika baki nakoma kwa sasa nina maisha yangu nashangaa cmu za vitisho kwa watu tofauti tofauti nakubali kufa ila kama Mungu atapanga, na navijuwa vingi kuhusu yeye nikisema kuongea nitampoteza afanye mziki ale ujana mimi nakula shida aniache..."
Pia akaongezea kwa ujumbe huu " Na Arusha kwa mama alienizaa tambuweni nasakwa Mererani Manyara nitapigwa bastola niayo tu!!!"
Mwisho kabisa akatoa baraka zake " Mungu ambariki sana awe na uwezo naenda kuchukuwa arabii yake muda cyo mwing kutoka sasa.!!"

Mkasa huu ndio umempelekea Suddy kutokuonekana maeneo ambayo Nay anajua huwa anapatikana kiurahisi na kuamua kuishi mbali na Jiji la Dar es salaam.

Na hii ndio RB ya Nay - K/RB11782014
Tarehe 25/04/2014

Mpaka dakika ya mwisho habari hii ikipanda kwenye Website.Blog yetu hatujafanikiwa kumpata Nay na kusikia kutoka kwake.
 
hyo nay hajakutana na ngumi jiwe..kzi kuonea wabana pua tu...na tatoo zke feki
 
Acheni kujipa promo za kijinga ili kupewa tension..utoto huo mnaofanya mxuuuuuu!!
 
house boy amedumu kuishi na mwanaume mwenzie kwa Miaka mitano?.. na bado ana hamu ya kuendelea kumpikia? aisee!..ukisikia uhan.thi ndio huo
 
Kwa hiyo picha ya ney nimeamini ile scandal
make wale wakipiga picha lazma waoneshe hiyo mishipa inayoelekea down
 
nilijua kamkamata Dogymasta13 wa instagram, maana kasema anamtafuta vibaya mnoooo
 
Kwa hiyo picha ya ney nimeamini ile scandal
make wale wakipiga picha lazma waoneshe hiyo mishipa inayoelekea down

Kile kidemu chake kina mimba ki Siwemaa yaan sijui yake sijui ni ya mababuu
 
Alimfanyaajee

sindo alipost picha na video ya siwema akivalishwa pete ya uchumba na obasanjo? the next day aka post picha za siwema akiwa uchi, and much more harm than good...
 
sindo alipost picha na video ya siwema akivalishwa pete ya uchumba na obasanjo? the next day aka post picha za siwema akiwa uchi, and much more harm than good...

Kumbeee lol
 
Kwahiyo jamaa alikuwa mpishi wa Ney(haha).Anyway huyu Ney kutakuwa na vingi nyuma ya pazia ambavyo hatuvijui kutoka kwake,juzi tu nimesikia story ya utekaji akiwa kwenye 'ikulu' yake kimara,leo tena naisikia hii story redioni na jamaa anasema kunasiri nyingi anazijua kuhusu Ney ndo maana anamuhofia.Huyu nahisi atakuwa jambaz tu tena
 

Pengine ni cameron
 
Hiyo picha bastola kama ya kike eti??
Haijaendana na ukauzu anaojifanya anao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…