Ney wa Mitego atoa kauli ya kumfananisha mkewe aliyemzalia watoto watatu na bahasha

Ney wa Mitego atoa kauli ya kumfananisha mkewe aliyemzalia watoto watatu na bahasha

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,325
Reaction score
2,491
Mwanamuziki wa bongo flavor ajulikanaye kama Ney wa Mitego ametangaza kuwa baada ya kujipatia watoto watatu, hana tena mapenzi na mama watoto hao bali ana mapenzi na watoto hao.

Kwa kauli hiyo, ni sawa na mama watoto hao kuchukuliwa kama bahasha maana bahasha ikishafikisha barua, inakuwa haina umuhimu tena bali kinachofanyiwa kazi ni barua iliyokuwa ndani.

Binafsi kama mwanaume sikufurahishwa na kauli kama hii kwamba hataki mazoea na mwanamke bali mapenzi ni kwa watoto, na je kama si huyo mwanamama hao watoto angeweza kuwazaa mwenyewe.

Huu pia ni ujumbe kwa wale wenye tabia kama za huyu jamaa na pia wale wanaotelekeza mama na watoto wanaenda kutafuta mwanamke mwingine.

Mtoto anahitaji malezi ya wazazi wote labda itokee bahati mbaya mmojawapo kafariki lakini unakuta mtoto anateseka, pimbi anadunda mtaani.

Je wewe unamwunga mkono Ney wa Mitego kwa kauli yake.
 
Ney wa mitego kuna wakati hua anajitoa ufahamu...sishangai kama ametoa meneno kama haya
 
Katika wanamiziki waliookota dhahabu kariakoo huyu ni mmoja wapo, hana kipaji na kichwani zimepungua. Hata sijui anaimba miziki ya aina gani. Pia kuchapiwa kunauma sana, anaishia kubwabwaja.
 
Kwahiyo unataka aoe wake watatu?after all hao baby mamaz wake ni viguu na njia hivyo kaona bora alee mwenyewe wanae kuliko watoto kutwa kuletewa akina uncle.
 
Kwahiyo unataka aoe wake watatu?after all hao baby mamaz wake ni viguu na njia hivyo kaona bora alee mwenyewe wanae kuliko watoto kutwa kuletewa akina uncle.

angeoa basi ndipo azae.
 
ktk wanamiziki waliookota dhahabu kariakoo huyu ni mmoja wapo, hana kipaji na kichwani zimepungua. Hata sijui anaimba miziki ya aina gani. Pia kuchapiwa kunauma sana, anaishia kubwabwaja.

Huenda na yeye anatumia usupperstar wake kuchapa ndo maana anachapiwa.
 
Kwa style hii Tanzania ijikwamue kwenye vita ya umaskini na ujinga kweli? Lord have mercy.
Yani wewe ndio umetafsiri kutokana na maono yako, alafu unene yakua yeye ndio kanena.
 
ktk wanamiziki waliookota dhahabu kariakoo huyu ni mmoja wapo, hana kipaji na kichwani zimepungua. Hata sijui anaimba miziki ya aina gani. Pia kuchapiwa kunauma sana, anaishia kubwabwaja.

Wanasema hajaokota dhahabu bali na yeye anauza haramu!
 
Kwa hiyo kinywa cha ney wa mitego kilitamka neno bahasha au wewe ndio umetoa tafsiri zako????

Mkuu hii ni Shida zaidi ya Tatizo. Hebu vuta Picha ndio mwalimu anamfundisha mwanao, ambaye wewe unahangahika kwa kuvuja jasho kutafuta ada mwanao atoke kwenye ujinga kumbe ndio anaingia rasmi kwenye Giza la ujinga kuelekea upumbavu.
 
Ana demu wake maeneo ya gedeli mwanza anafanya kazi ktk shirika la ndege fulani bahati mbaya huyo dada ni mwathirika
 
Tangu Huyu Jamaa Alipoimba Kuwa Ni Rafiki Wa Lucifer,tena Huwezi Kwenda Mbinguni Bila Yeye,niligundua Ni 'Insane' Kabisa.
 
Kuna jamaa mmoja jina(WINME) katoa komenti ambayo imenitishaaa.. mwanangu kama kweli hali mbaya.naogopa kinoma haya mambo nandomana nikipata demu maeneo mapya na tangaza kama chizi vile lengo kupata data zake japo waswahili wanasema ukimchunguza bata huwezi kumula .
 
Back
Top Bottom