Neymar bado taa hazija kumulika wewe

Neymar bado taa hazija kumulika wewe

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
3,415
Reaction score
2,043
NEYMAR BADO TAA HAZIJA KUMULIKA WEWE.

Na Haatim Abdul.

Tumezoea mtu akipanda stejini taa ziwe zinammulika yeye kwa maana ya kwamba ndiye kituo kikuu cha umakini kwa hadhira. Neymar Jr alipoona kuwa kivuli cha Messi kinamkinga na taa anayoitaka immulike akaamua kutimkia kwenye jiji la kifahari la Paris kujiunga na PSG lakini kusema ukweli sijaona bado kama timu inacheza kwa kumzunguka zaidi yeye na kumfanya awe ndio mfalme kama anavyotaka. Bado yani.

Anachotaka zaidi mbrazili huyo ni mafanikio binafsi ambayo ni wazi asingekaa akiona akiyapata pale Barcelona. Na ndio maana malengo yake ni kuona timu ikicheza kwa kumzunguka yeye zaidi. Anachosahau Neymar ni kwamba hakuna mchezaji aliewahi kupata ufalme kwa mafanikio yake binafsi. Sana sana hichi ni kitu ambacho kitampa tuzo nyingi.

Ufalme ni zaidi tu ya kupiga watu kanzu na chenga za kutisha. Ufalme unaambatana na rekodi mbalimbali ikiwemo za ufungaji. Hawa wanaochongewa sanamu na wanao itwa wafalme hawakuwa tu wakipiga chenga watu 3 kwa wakati mmoja. Hapana! yule pale Ronaldo De lima alifanya makubwa pale Real Madrid lakini haikutosha kumfanya awe mfalme wa Bernabeu. Ronaldinho alifanya makubwa ya ajabu lakini ukifuatilia kwa kiasi kikubwa yalimsaidia zaidi katika kumpa mafanikio binafsi ikwemo Ballon D'or mbili lakini sio kama sehemu ya kuacha rekodi pale Barcelona.

Wanachofanya sasa hivi Messi na Ronaldo ndio ufalme kwenye klabu zao. Kuweka rekodi mbalimbali kwenye vilabu vyao ikiwemo nyingi za ufungaji. Mafanikio binafsi yangewapa tuzo sio ufalme. Ufalme huwa hauhitaji tuzo bali alama. Alama gani? Alama binafsi ya kukumbukwa kwa kitu fulani klabuni kama rekodi jambo ambalo Neymar bado hajalifanya.

Wakati anatua PSG hili la ufalme lilikuwa ndio hoja lakini watu walisahau kuwa kuna mtu tayari ambae amewapa furaha mashabiki wa timu hiyo na ni wazi bado hakuwa amekaribia kuvunja rekodi lakini kwa sasa amekuwa tayari kufanya hivyo.

Juzi kwenye mchezo dhidi ya Dijon mashabiki wa PSG walimzomea Neymar. Kisa? Alipiga penati ambayo ingeweza kumfanya Edinson Cavani kuwa mfungaji bora wa muda wote klabuni hapo. Kitendo cha mashabiki kumzoea Neymar kinaonesha kuwa wanathamini zaidi majukumu ya Cavani uwanjani na kile ambacho amekifanyia klabu hiyo kwenye ufungaji wa mabao.

Mchango wa Neymar ni mkubwa lakini rekodi ya mabao ya Edinson Cavani ni kitu ambacho kitaenziwa kwa miaka mingi ijayo. Kwenye swala la ufalme sasa hapa PSG kwa Neymar tayari changamoto imekuwa ni Edinson Cavani. Jiulize Messi na Ronaldo wana nini baina yao linapokuja swala la ufungaji mabao klabuni kwao. Ni ufungaji bora wa muda wote jambo ambalo hata Cavani alielekea kulifanya lakini Neymar akalichelewesha.

Bado Cavani anaweza kufanya hivyo na kwenda mbali zaidi lakini kwenye usiku ambao angeweza kufanya hivyo kwa jukumu ambalo mashabiki wengi wanajua ni lake halikuwa jambo ambalo mashabiki walilipenda hasa ikizingatiwa kuwa Neymar tayari alikuwa kwenye hattrick.

Neymar anapaswa kutambua kuwa ufalme hauji kwa chenga za maudhi na uhamisho wa kufuru bali kwa rekodi mbalimbali ikiwemo ile kubwa ya kuwa mfungaji bora klabuni. Kwa hali hio ni wazi kuwa machoni mwa wengi pale Parc des Princess, Edinson Cavani amekalia kama mfalme wao na Neymar ajue kuwa taa bado hazijammulika yeye na inabidi iwe ni zaidi ya vitobo na chenga za mwili bali rekodi binafsi zitakazo acha kumbukumbu klabuni
 
umeandika vizuri mkuu, Neymar anaforce hili awe mfalme kitu ambachoa anakosea
 
Hadi messi astafu arudi sayari yake ndo neymar tutamuona
 
Huyu kijana aje tu madrid. Taa zote zitawaka hadi zilizokua zinafifia zitammulika yeye tu
 
Back
Top Bottom