NFRA itulipe Wakulima wa Mbinga (Ruvuma) tuliouza Mahindi, ukimya wao ni maumivu kwetu

NFRA itulipe Wakulima wa Mbinga (Ruvuma) tuliouza Mahindi, ukimya wao ni maumivu kwetu

Mzee wa Code

Member
Joined
Sep 23, 2024
Posts
61
Reaction score
91
Mimi ni Mkulima kutoka Mbinga mkoani Ruvuma, nimekuja mbele yenu nikiwa na changamoto ambayo kwa imani yangu najua kupitia nyie naweza kupata msaada ambao kimsingi sio tu utanisaidia pekee yangu bali sisi sote wenye hii changamoto.

Naomba sauti hii ifike kwa Wizara ya Kilimo na ngazi ya juu ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Kumekuwa na tabia ya ucheleweshwaji wa malipo ya mahindi ambayo tunauza kwa NFRA, jamani imepita miezi miwili sasa, tumeuza Mahindi yetu lakini mpaka leo imepita miezi miwili malipo bado changamoto.

Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa msimu mpya wa kulima umeanza tukiwa hatuna mitaji ya kueleweka kwa kuwa mitaji yetu yote tumeipeleka kule NFRA, tukiamini kama pindi tutakapolipwa basi tunarudi tena shamba na shughuli zingine kuendelea.

Wengi wetu tunategemea kilimo kitutoe katika Maisha lakini NRFA wapo kimya kila tukienda tunapigwa kalenda bila majibu ya msingi.

Kwa kawaida NRFA huwa wanafunga vituo pindi muda wa mauzo unapomalizika, sasa hivi wamefunga kituo cha huku kwetu, tukiwapigia simu hawapokei, tukienda kuuliza kwenye kurasa zao za Mitandao ya Kijamii napo hakuna majibu sahihi.

Kuna tetesi kuwa wanataka kuwalipa kwanza Wakulima wanaodai malipo kidogo, wale tunaodai malipo kuanzia Sh milioni 10 tuendelee kukaa benchi, kama ni hivyo tutatoboa kweli kimaisha kwa staili hiyo?
 
Halafu wanatutaka tuwe wazalendo kwenye nchi ambayo wao wenyewe siyo wazalendo,huu ni utapeli unachikua mahindi ya mtu miezi mitatu hujamlipa una tofauti Gani na kibaka?lipeni Hela zetu,acheni ukibaka
 
Nfra walitoa bei gani kwa kilo?
Je madalali wa mtaani walinunua kwa bei gani kwa kilo?
 
kwenye bulimia hawapo Ila kuuza unamuona dc, rc na wangen Kibao Kutoka wizarani Dodoma wanakera sana
 
Endeleeni kuchagua ccm na kuwachezea ngoma viongozi wao wanapokuja kuwatembelea
Hapa ndio pale kenge anasimangwa kwakuwa sii msikivu wala mwelewa wa mazingira yake yanayomzunguka na kuwa ndio mateso yake.
 
Labda nyie wenye hela kubwa ndo hamjapata, mbna binamu yangu kapata hela yake 3.5M week ya 2 sahiv

Hebu fuatilia vizuri.
 
Back
Top Bottom