NFRA wanachelewesha malipo ya mauzo ya mahindi kwa wakulima

NFRA wanachelewesha malipo ya mauzo ya mahindi kwa wakulima

Clark boots

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2017
Posts
6,770
Reaction score
6,202
Ndugu Watanzania, ikimbukwe kuwa mwezi July serikali ilitangaza kununua Mahindi kwa wakulima kupitia wakala wa hifadhi ya chakula "NFRA" ila kitu kinachoshangaza na kustaajabisha ni kuwa malipo yanachelewa sana, wakulima wanakaa zaidi ya wiki tatu hali ya kuwa fedha zilishatengwa tayari.

Uhalisia ni kuwa, wakulima wengi tunahitaji fedha ili tuweze kununua pembejeo mapema ili kujiandaa na msimu mpya wa kilimo 2024/2025, halikadhalika pesa hizo tunazitegemea kulipia madeni yetu na kujikimu kimaisha ila bado pesa zinacheleweshwa.

Wizara ya Kilimo tunaomba mtusaidie wakulima maana tunaishi kama digidigi, tulipwe pesa zetu kwa wakati. Kwanini NFRA mnachelewesha malipo ilhali pesa za kununulia Mahindi yetu zilikwishatengwa kitambo sana. Maisha haya ni PESA, bila PESA maisha hayaendi kabisa.
 
Back
Top Bottom