Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mwenge wa Uhuru Wilayani Ngara umetembelea na kuzindua Mradi wa Maji Wenye Thamani ya shilingi Bilioni tatu chini ya Ufadhilii wa Benki ya Dunia kupitia LADP (Local Area Development Program) inayosimamiwa na NELSAP (Nile Equatorial Lake Subsidiary Action Program).
Mhandisi Simon Ndyamukama Meneja wa Wakala wa Usambazaji, Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) ameeleza kuwa Mradi huo unahudumia Wananchi zaidi elfu 5,000 wa Kijiji cha Rusomo Mradio hua ulianza Rasmi Mwaka 2020.
Muhandisi Ndyamukama amesema pia Mradi huo umetekelezwa na Mkandarasi M/s ECIA CO. LTD JV ABEMLO CONTRACTRS CO. LTD kwa Mkataba wenye Tsh Bilioni tatu.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Ndaisaba Ruhoro ameipongeza Serikali ya Awamu ya sita Chini Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuwezesha na kuhakikisha Mradi huo unakamilika kwani Wananchi wa kata ya Rusumo na sasa wataanza kutumia Maji safi na Salaama.
Wakati huo huo Mwenge wa uhuru ukiwa Wilayani Ngara umepitia jumla ya Miradi 7 na shughuli 9 zenye thamani ya shilingi Bilioni 5,162,001,623.60 na umekimbia Umbali wa Kilomita 66.
Itakumbukwa kuwa ujumbe wa Mwenge wa uhuru 2024 ni Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uhifadhi wa Mazingira wenye Kauli mbiu isemayo "Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa endelevu.
Attachments
-
Screenshot 2024-09-23 at 20-12-38 Kharidi Abdul (@kageradigital) • Instagram photos and videos.png927.7 KB · Views: 3 -
Screenshot 2024-09-23 at 20-13-54 Kharidi Abdul (@kageradigital) • Instagram photos and videos.png777.3 KB · Views: 2 -
Screenshot 2024-09-23 at 20-14-41 Kharidi Abdul (@kageradigital) • Instagram photos and videos.png829.1 KB · Views: 2 -
Screenshot 2024-09-23 at 20-15-14 Kharidi Abdul (@kageradigital) • Instagram photos and videos.png776.3 KB · Views: 3 -
Screenshot 2024-09-23 at 20-15-00 Kharidi Abdul (@kageradigital) • Instagram photos and videos.png788.3 KB · Views: 2