Ngasa kwenda west ham!!

Akamuulize mohamed mwameja;na hussein masha
ushauri

kabla ya kuondoka ajifunze kuchuma machungwa ingawa kule atakutana na matunda itamsaidia kuona kama kazi ya kawaida na si utumwa


....aaaarrrgggh sweetbaby, Husseyn Marsha yeye kaja kutafuta maisha tu, habari ya mpira kesha sahau, au umemchanganya na Athumani China aliyekuwa kwenye majaribio Reading?

Mwingine Athumani Machupa, ambaye alishindwa majaribio hata na timu ya Hounslow Borough, (bongo ni timu kama ya tandika mabatini!)
 
Kazi ipo hapa, namshauri mdogo wangu Ngasa aanze intesive tuition ya English manake huko kwenye website ya Homeoffice nimekutana na kali nyingine kwenye requirements- "must be able to demonstrate basic english skills" na kama ana mke hii inapply kwake pia!. Sasa sijui mdogo wetu kaishia kidato gani.

Pia uzushi mwingine ni kuwa ni lazima awe amecheza 75% ya mechi za Stars katika miaka miwili iliyopita kabla ya tarehe ya kusubmit hiyo application, sina hakika kama anakidhiki kipengele hiki. Kigezo hiki kilimkumba Yakubu na jamaa mmoja wa Zambia lakini walikubaliwa baada ya ku appeal kwa kisingizio kwamba walikuwa hawaivi na makocha wa nchi zao ndo maana hawakuweza kufikisha hicho kiwango.

Na kama nilivyosema awali kuna kigezo cha FIFA ranking na kama unatokea nchi ambayo ipo chini ya 70 hupewi working permit. Kuna mchezaji mmoja wa Chile Liverpool walimpenda lakini walipoingia Home Office wakatoswa kwa kuwa by then nchi yake ilikuwa ya 72 kwenye ranking.

Aende akajaribu tu labda miujiza itatokea, tena tumuombee sana.
 
Mkuu njoo na fact tuwekee hizo sheria za uhamiaji za UK zenye masharti kama unayoyasema..........
 

mkuu hicho kigezo cha english sidhani kama kina umuhimu mkubwa!muulize vidic kama alikuwa anaongea english alivyokuja england!,u can learn it ukiwa ushasajiliwa.,tatizo ni hapo kwenye ranking,ila kama dogo atapiga soka safi watamsajili then watamweka mahala kwa mkopo,after 3yrs napata EU passport,then evrything will be ok!!.tatizo wachezaji wetu hawajifui vyakutosha kabla hawajaenda kwenye majaribio.akina henry joseph vipi??and ndo kishalia?
 
mkuu hicho kigezo cha english sidhani kama kina umuhimu mkubwa!muulize vidic kama alikuwa anaongea english alivyokuja england!,u can learn it ukiwa ushasajiliwa.

Kaka hii shreria ni mpya, I think ilikuwa introduce mwaka jana mwishoni wakati hao kina Vidic washasajiliwa, imekuja wakati hapa UK walipo introduce point based system, foreign footballers wanaangukia kwenye tier 2, fanyeni research wandugu, hizi info zimo humuhumu mtandaoni.
 
Mkuu njoo na fact tuwekee hizo sheria za uhamiaji za UK zenye masharti kama unayoyasema..........

Hizo nilizoweka hapo ndio facts unless wewe uwe una definition tofauti ya neno 'fact'. Au mpaka uone hayo nilosema yameandikwa na mzungu ndo utaamini kuwa ni fact?
 
kwa maana hiyo kama wewe u mtanzania hata uwe unakipiga kama Pele- visa hupati.

I should correct myself on this,I should have said 'work permit hupati'. VISA utapata ya kuja kufanya majaribio na clubs husika zina weza kukubaliana transfer fee na mchezaji akakubali personal terms lakini kizingiti kikawa huko home office, wao ndo wa mwisho.
 
acheni kumvunja moyo ngasa,lazima muelewe kuwa mpira wa afrika umepanda na wachezaji wana vipaji hivyo kwa ngasa kucheza ulaya anaweza kama alivyoweza shabani nonda.
kwa suala la kuwa eti atapata kipingamizi kwa kukosa kibali kwa sababu nchi yetu ipo chini ya kimpira duniani hiyo sio issue kwa sababu timu za hapa kitu wanachofanya ni kuwapeleka wachezaji waliofuzu majaribio kwenye nchi kama portugese au uswis kwenda kucheza ligi za huko mpaka atakapofuzu vigezo vya kupata visa ya hapa uk,mfano mdogo ni kwa manucho wa mozambique,mnaweza kuniambia msumbiji rank yake fifa ni ya ngapi?....suala la lugha sio big deal,wala hawaangalii una degree ngapi,hata ukiwa na basic wao wanakupa,wasichotaka kwa sasa ni suala la kutafuta wakalimani ambalo linawaingiza gharama nyingi kwa mwaka......MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU MBARIKI NGASA
 
wabongo bwana..... wamekaa kujiliwaza tu! badala ya kufurahia wao wanaona haiwezekani na haitawezekana!! Ngassa anaweza akasajiliwa, lakini akawa yuko kwenye soccer academy ya club husika na hata kukopehswa kwa club nyingine yeyote nje ya UK (lakini Europe) na akatimiza vigezo ambavyo vitamwezesha kucheza EPL! Ni kama issue ya Thabeet!
 
mkuu manucho katokea angola!!
 
....suala la lugha sio big deal,wala hawaangalii una degree ngapi,hata ukiwa na basic wao wanakupa,wasichotaka kwa sasa ni suala la kutafuta wakalimani ambalo linawaingiza gharama nyingi kwa mwaka......MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU MBARIKI NGASA

...ebwana eeh,

kiingereza sio big deal Bongo, lakini nchini kwa watu ushaambiwa wenyewe hawataki!

May 7, 2008

Foreign footballers from outside the EU will be barred from joining Premier League clubs from October unless they can speak simple English under new immigration rules.


...ndio maana nikauliza Ngassa ana umri gani? maana soccer academy UK ni baina ya 16-19yrs olds...
 
mkuu manucho katokea angola!!

nimekupata kaka,aksante kwa kuniweka sawa,kwa sasa angola rank yake fifa ni ya 78,hivyo utaona jinsi ngasa anaweza cheza uingereza.
 
View attachment 3957

View attachment 3958

View attachment 3959

TFF Secretary General, Fredrick Mwakalebela said Ngasa has to prepare well if he wants to meet professional standards.
The two-week trials would start from April 13 and end in 25.
Mwakalebela said Young Africans and the teenager should not waste this chance.
"The golden chance has finally come, they should use it wisely as we are behind them," said Mwakalebela.


 
...ebwana eeh,

kiingereza sio big deal Bongo, lakini nchini kwa watu ushaambiwa wenyewe hawataki!





...ndio maana nikauliza Ngassa ana umri gani? maana soccer academy UK ni baina ya 16-19yrs olds...

nani amekwambia ngasa hajui kiingereza?we unafikiri kufanya TOEFL ni kama kuchukua course ya miaka 3?hicho ni kitu rahisi sana kwa mtu mwenye nia na mwenye kuangalia mbele.ulaya sio mbinguni,sheria zipo na wanaendelea kuzitunga na watu wanazitimiza vilevile
ngasa umri wake ni U23 na haji ulaya kujiunga na academy,analetwa na wakala anayetambuliwa na fifa,
 
mfano mdogo ni kwa manucho wa mozambique.

Huyu dogo alisajiliwa na Man U moja kwa moja kutoka Petro Atletico ya Luanda na mara ya kwanza alitoswa hiyo work permit kwa kuwa alikuwa ha meet hizo criteria, ndo maana jamaa wakampeleka Panathianaikos ili aweze kugain hiyo qualification.
 
Hakuna mtu anayemkatisha tamaa huyu dogo hapa, am sure West Ham wako aware na hizo criteria and they must have a good plan with him. Imebidi tueleweshane hapa kwa kuwa naona baadhi yetu tumekuwa over excited kuwa tutakuwa na mchezaji kwenye PL, this might take up to 3 years. Tumtakie kila la heri tu afanikiwe.
 
Dogo ana future nzuri inatakiwa aandaliwe mapema,hili la rank hata kama unaenda kucheza league daraja la pili ni lazima au ni premier league tu
 
Hizo nilizoweka hapo ndio facts unless wewe uwe una definition tofauti ya neno 'fact'. Au mpaka uone hayo nilosema yameandikwa na mzungu ndo utaamini kuwa ni fact?
Acha kauzibe kijana....umesema sheria eti sijui nini kuwa ukitaka kucheza EPL uwe katika fifa ranking za 70........tupe link au paste sheria hizo sio maneno ya vijiweni bar.....
 
Acha kauzibe kijana....umesema sheria eti sijui nini kuwa ukitaka kucheza EPL uwe katika fifa ranking za 70........tupe link au paste sheria hizo sio maneno ya vijiweni bar.....

Couple of stories

Source


Habari kamili Home Office rejects Man City move for Iraqi hero midfielder Nashat Akram | Manchester City - Times Online
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…