Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 752
Wakati anaondoka nchini, Nizar alikuwa mchezaji wa Mtibwa Sugar na hajawahi kuchezea zile timu zetu na ndo maana hata kwenye Stars anapogusa mpira watu hawashangilii. Huo ndo mfumo madhubuti wa soka Bongo tunaojaribu kuomba kwa Muumba kila kukicha ubadilike lakini wapi!Hiyo mechi ilikuwa ni friendly ndio maana uliona half time wamebadirisha timu nzima, kwa hiyo huwezi kutegemea kuwaona wakicheza kama wanavyocheza kwenye mechi za ligi. Muda aliopangwa Ngassa ni mfupi sana hopefully atapata muda zaidi wa kufanya majaribio na jamaa. Juzi timu ya Nizar Khalifan ilicheza na Manchester City naona hakuna aliyezungumzia.