Ngoma imenoga leo mrs amekuja na vipimia H.I.V

first time mnataka kujipima nyumbani? bila ya ushauri nasaha? kweli nyie mnatafuta suicide.....
shauri yenu

haha haha haha,mkuu FP,kweli kupima ni ishu nyingine
 
Wakubwa habari zenu jamani mashauri yenu niliyasoma vilivyo nikawa najitahidi kumweka mwenzangu sawa ikawa kama mimi nagwaya lakini kuna mkuu alifanya kuni pm nikamwonyesha mwenzangu akakubali kwa shingo upande usiku tulilala huku kilio cha kwiki kimetawala chumbani kwetu. Kulipo kucha tukawa tumetembelewa na kaka yangu kwa hali aliyoikuta nyumbani iliniita chemba na akataka kujua nini kinaendelea nikamjuza kilakitu, akanihoji me naogopa nini kwenda kupima jibu nikawa sina akanishawishi kwa maneno yenye kutia moyo na yenye ujasilri kweli akatuchukua mpaka Victor clinic tukaonana na mshauri akatupa nasaha. Na baada ya mda tukachukuliwa damu natukarudi upande wa mapokezi yule bingwa wa mashauri hakutuacha aliendelea kutupa kampani ki ukweli mwili wangu haukuwa na fulaha hata kidogo hofu tu! Ndio ilikua imenitawala. Mda ka wa dakika 28 mshauri akaitwa na doctor kisha mshauri akatuita aisee kizungu zungu nilichokipata halimnasura nizimie basi tukaanza kupewa maneno tena nikjua tumekwisha but after conciling majibu tuliyopewa. Yalionyesha Negetive kwa vipimo vyote yani Ungold na. Determine sikuamini masikio yangu mpaka pale wife alivyokuja kunikumbatia kwa kilio huku akiniomba msamaha kwa kunihisi vibaya
Kiukweli mwaka jana nilikua na mahusiano na kabinti fulani hivi bahati mbaya yule binti aliugua TB mwili wake ulidhoofika sana kiasi cha kwamba watu wengi wanajua ni HIV habari hizi zikaenea kwa kasi ndio mpaka kumfikia mama mtoto wangu nadhani kwa hali aliyomwona nayo yule binti ilikua lazima afikie hatua hii, kiukweli wife ni mwelewa na alianza mda mrefu sana kuzungumzia hili swala na mimi kwa hofu nikawa napiga chenga mpaka akafika hatua ya wife kinunua hivyo vidude,,
Baada ya kupima nimejifunza kitu kwamba uaminfu ni silaha ya kumshinda pepo ngono tamaa ni mbaya tena sana kama una mke tulia namkeo hivi vibinti vinavyoo zagaa na vimini sketi vyao vinahangaika kuvunja ndoa zetu.
Nitamuheshimu mke wangu na kumlinda mpaka kiama cha maisha yangu
Asanteni sana Jf members.
 
duh! umetisha Bob Jay! Sasa weka mkakati wa kumkabili SHETANI kwani hii stori yako naye ameshaisoma na atakuzungukia tena, probably kwa staili tofauti kidogo (kama kawaida yake).
 
duh! umetisha Bob Jay! Sasa weka mkakati wa kumkabili SHETANI kwani hii stori yako nay ameisoma na atakuzungukia tena.

kila kitu kina kinyume chake
Moto>baridi
Kilio>kicheko
Fulaha>huzuni
Mungu>shetani
Kumbuka hayo yote huambatana nipo tayari kwa mapambano na adui shetani na Mungu atanisimamia vita hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…