Ngoma isiyo kelele

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Ngoma hii ngoma gani, ngoma isiyo kelele
Wanaicheza kwanini, pasipo vigelegele,
Majasho yote ya nini, bila ngoma na kengele,
Sichezi miye sichezi, ngoma isiyo kelele!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Ngoma hii ngoma gani, ngoma isiyo kelele
Wanaicheza kwanini, pasipo vigelegele,
Majasho yote ya nini, bila ngoma na kengele,
Sichezi miye sichezi, ngoma isiyo kelele!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)


sio sauti Za vijiji kama ilivyo sauti Za umeme maana kam awako wengi tehe tehe tehe ,dont take it seriously
 
Hahhahhahaha! Ngoja nicheke kwanza!

Ngoma imenoga!! watu busy!!
Ngoja kila mtu anacheza!! watu busy!!
kimya kimya!! watu busy!!
watu wacheza sasa!! watu busy!!
'
'
'
tungoje tuone!! ubusy uko wapi jamani!!
 
Kelele za nini kwa ngoma ya mjini,

Pale mdundo na hapa ngurumo ndo zilo yakini,

Kelele si wakatiwe wajuzi wachache ndo watabaini,

huchezi weye mdundo kisa u wa ya sabini,

zetu sie wa sayansini kimya kimya iso walakini,
Ukelele ukelele je? Waamke wafitini?

Ngoma yetu hii matawini ya kelele chezeni nyie wa mzizini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…