Ngoma mpya ya ‘nataka kulewa’ ya msanii ‘diamond’, yadaiwa inamhusu ‘wema sepetu’ kwa asilimia mia…!

Ngoma mpya ya ‘nataka kulewa’ ya msanii ‘diamond’, yadaiwa inamhusu ‘wema sepetu’ kwa asilimia mia…!

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
diamond1.jpg

MSANII anayeshikilia nafasi ya juu kwa sasa kwenye muziki wa kizazi kipya Tanzania Nasseb Abdul ‘Diamond’, inasemekana kuwa ameamua kutoa ya moyoni juu ya Wema Sepetu katika ngoma yake mpya ya ‘Nataka Kulewa’, ambayo imezungumzia matukio yote yaliyomkuta alipokuwa na mwanadada huyo na mengine ambayo yalikuwa yanazungumzwa na watu pindi wakiwa wapenzi.

Chanzo kimoja cha karibu na msanii huyo kilizungumza na DarTalk, kilidai kuwa mistari yote inayopatikana ndani ya ngoma hiyo ni matukio ambayo Diamond alikuwa ameyafanya kwa Wema na mengine ya kusikitisha ambayo awali yalikuwa yanazungumzwa na yeye alijua uzushi.

Chanzo hicho kilidai kuwa Diamond ameamua kutoa ngoma hiyo ili itoe ujumbe kuwa yote waliyokuwa wanafanya ni ujinga wake na anashukuru kwa kumfanywa kama zezeta katika mapenzi yao kwani alikuwa anaambiwa lakini hakusikia.

Baadhi ya maneno yanayopatikana ndani ya ngoma hiyo yanasema kuwa ‘mwanzo sakuamini nilijua vya kuzua, kumbe mjinga ni mimi ninayetunza wenzangu wanachukua, mapenzi mapenzi yalinifanya niliye vibaya kama mtoto, yaliyonikuta niache niseme yamenikaa moyoni.’

Mengine ni ‘nikamvisha na pete ya kumuoa kukata vilimilimi vya wazushi na wanafiki wanaomponda, kumbe mwenzangu na mimi ni bure tu najisumbua, sisi tupo kama 20 mabuzi, ving’asti na wengine wa anawahonga,’ ni baadhi ya maneno mazito yanayopatikana ndani ya ngoma hiyo

Kutokana na baadhi ya maneno hayo ukiyafuatilia mapenzi ya Diamond na Wema yalivyokuwa utajua ni maneno ambayo yamejaa ukweli juu ya mahusiano yao ambayo yaliteka watu wengi hasa pale alipomvisha pete Wema.
 
Ndio kina nani hao?

masuper star wa bongo,wanaowezesha magazet ya udaku kuuzika punde habari zao zinaporusha,wanawaweka waandish wa habari wa udaku mjin,sababu habari zao zinasaidia familia zao waandishi kwenda choon
 
masuper star wa bongo,wanaowezesha magazet ya udaku kuuzika punde habari zao zinaporusha,wanawaweka waandish wa habari wa udaku mjin,sababu habari zao zinasaidia familia zao waandishi kwenda choon
asante ndugu Money stunna na mie nitaanza kufuatilia hayo magazeti inaonekana nakosa uwondo mkubwa sana
 
Last edited by a moderator:
Money stunna na wewe kama nakufananisha na yule mwandishi wa lile gazeti la udaku...
Maanake unavyotiririka na sridi za hawa mastaa inaonekana unafahamu kweli na ni mzoefu,
 
Back
Top Bottom