Wakati mwingine nasi twachangia wakati unamnyima mtu haki za kimsingi kwa madai ya kuwa leo nimechoka huku mwenzio akuhitaji.......au kuna jambo lile hakulifanya utakavyo sasa malipizi wakati wake ni huu..............ataipata...............mwishowe mwandani wako naye ameamua kujitutumua kwa kujitafutia uhuru bandia na hivyo kuishia kutafuta majibu mteremko hata kule ambako hakustahili...........
Ruta watu wanaonyimana kwa makusudi, wanaokomoana kwa kutowaelewa wenzao iwapo kuna sababu ya msingi kuomba mapumziko ndio hao waliojisalimisha. Usitegemee mtu aliyejisalimisha kwako ajali sana hisia zako.
unamwacha na shombo lake>>>
mbona waniogofesha hivyo..........sasa utawatofautishaje makundi hayo mawili?
Sio nakuogopesha Ruta ila ukweli ndio huo. Wengi wanaolalamika kwamba wana hayo matatizo lazima mmoja wao awe haridhiki na mwenzake.
Inabidi ujitahidi kuwa makini tu, msome mtu kama unavyosoma kitabu unapotaka kujifunza kitu kweli na sio ili ukariri.
wengi ni wanafiki machoni ukiwepo wanaficha makucha baada ya kuanza safari nao huja kukuparua nayo...............halafu utashangaa hivi huyu nilifikiri ninamjua kumbe yuko vingine.......tayari hayo ni maumivu makali anakuachia.........lol
Inabidi sasa na wewe uwe mjanja.
Tatizo lenu nyie nanyi hua hamsubiri hata muwe marafiki na mabinti, mnakimbilia tu kutangaza 'ohhh nakupenda' mara 'nakutaka'. Kwa style hiyo unadhani hatoficha makucha ili akukamate vizuri? Niliwahi kuanzisha thread kuhusu haya mambo. . . ukitaka mtu awe muwazi kwako kuwa rafiki yake kwanza, mambo ya kutongozana yaje baadae sana bila kutarajiwa.
hili ni kweli ukiona hata urafiki una mushkeli basi ujue mengineyo yatakuwa mabaya zaidi............mimi formula yangu ni kuwa kama tumeshindwa kuelewana kwenye mambo madogo basi makubwa itakuwa pata shika au mshike-mshike...........huamua kuishia wakati mwuingine hata siagi......................nikitarajia kubadilika kwa gia kutatoa ujumbe murua na unaojitosheleza.........
Hiyo nayo nzuri, ukishamsoma mtu anareact/act vipi kuhusu mambo madogo madogo unapata urahisi wa kujua kama mtawezana au la.