kwa kweli sikonge umenikonga moyo wangu vibaya mno
hizo video za wazaramo zinanikumbusha mbali sana wakati huo kila wiki mtaani kwetu chini ya miembe kulikuwa lazima kupigwe hayo magoma, vanga, chakacha na mkole(wawakinamama) ila kwenye mkole sie raha yetu ilikuwa kumwangalia mwali anavyonema tena wakati mwingine matiti yakiwa nje
mdundiko by then ndo ilikuwa mziki wa kiswahili hasa, wamama walikuwa wakiacha masufuria yanaungulia kisa kwenda kucheza mdundiko na
iwapo ngoma hiyo ikipita mtaani watoto hujikuta wakisombwa wakija kukumbuka wako kama kilomita mbili au tatu toka nyumbani na wakati mwingine hupotea
dah; kweli sasa twaishi dunia nyingine kabisa, vitu hvyo siku hzi watu hawavishabikii sana huku mijini labda huko pembezoni samvula chole,masaki,na kama alivyosema max kimanzichana