Ng'ombe 25 wafa baada ya kupata chanjo dhidi ya homa ya mapafu

Ng'ombe 25 wafa baada ya kupata chanjo dhidi ya homa ya mapafu

BestOfMyKind

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Posts
1,350
Reaction score
1,464
Dar es Salaam. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ameagiza kusakwa na kukamatwa kwa wataalamu wa mifugo, waliotoa chanjo ya homa ya mapafu kwa mifugo katika Kijiji cha Mlazo, wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano, Septemba Mosi 2021 na Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesema, Waziri Ndaki ametembelea kijiji hicho kuona madhara yaliyotokea na ameagiza wataalamu hao watafutwe na wafikishwe katika Baraza la Veterinari Tanzania kwa uchunguzi zaidi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa wataalamu hao wasakwe na kukamatwa kutokana na vifo vya ng’ombe 25 na madhara tofauti kwa mifugo mingine iliyochanjwa.

Amesema baada ya chanjo kuna ng’ombe walikuwa na mimba zikatoka na wakavimba sehemu walizochomwa sindano.

“Mbuzi mmoja alikufa, watano walivimba na walitoa mimba 12. Kwa upande wa kondoo waliokufa 20, waliovimba 16 na watano mimba zilitoka,” amesema Ndaki.

Ndaki amesema mchakato wa chanjo ya mifugo katika kukabiliana na magonjwa ina lengo zuri lakini amesikitishwa namna ya utekelezaji huo ulivyofanyika katika kijiji cha Mzalo kwakuwa hazikuzingatiwa kanuni za kitaalamu.

Waziri Ndaki ameiagiza kampuni ya Agristeps Limited iliyoingia mkataba na halmashauri ya wilaya ya Chamwino kwa ajili ya kusimamia mchakato wa utoaji chanjo kusisitisha shughuli hiyo na kufikishwa Baraza la Veterinari Tanzania kwa uchunguzi.

“Wale wataalamu waliochanja ng’ombe watafutwe majina yao, wamesomea wapi, wapelekwe kwa msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania. Kampuni ilitakiwa ijiridhishe na utaratibu na mchakato mzima wa uchomaji wa chanjo, isimama kutoa huduma,” alisema Ndaki.

Mbali na hilo, Ndaki amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha watoa huduma walioingia nao mikataba ya utoaji chanjo za mifugo dhidi ya magonjwa 13 ya kimkakati, yanafuata taratibu za utoaji wa huduma hiyo inayoendelee kote nchini.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa wa wizara hiyo, Profesa Hezron Nonga amesema uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa sindano zilizotumika kwa ajili ya chanjo kwa mifugo hiyo zilikuwa ndefu.

Chanzo: Mwananchi
 
Chanjo kama chanjo

Kukubalika ama kukataliwa hutokana na matokeo chanya(hasi)
 
Chanjo feki hizi, dah... wizara ya mifugo inaliongeleaje jambo hili?
Maana kwenye kilimo na mifugo ndiko kumekithiri uwepo wa madawa feki
 
Habari kama hizi zinanifanya nijitafakari mara 2.
 
Hahaaa bado ile ya UVIKO sijui itakuaje , mwenyezimungu atunusuru mhhhhhhhhh kwa sauti ya kipoozeo
 
Gwajima aingize hii kwenye mahubiri yake ya jumapili pale kwenye godown lake.
 
Back
Top Bottom