Mtondoli
Member
- Nov 9, 2021
- 70
- 174
Watu wa Kaya hii wana utaratibu wao, mpangaji hana sauti kwa mwenye nyumba katu, hawezi hata kupiga mluzi nje ya nyumba mbele ya mwenye nyumba, kwanini asione aibu kumpigia kelele mwenye nyumba?
Alipotia nia mwendazake aliwaomba wenye nyumba wampangishe kwa miaka kumi kisha atawarudishia nyumba kwa makubaliano ya kuiboresha zaidi, mwenye nyumba akashauriana na wanafamilia wakamwamini wakampa, loooh na kumbe mpangaji ni mbogo maji alipohamia tu kaanza kuwatimua kuanzia mwenye nyumba na watoto wake
Kila aliyejitambulisha kwamba yeye ni sehemu ya familia ya mmiliki wa nyumba alitimuliwa, mpangaji kwa kujihami akaleta watu wake, wengine kawakodisha kutoka nje wengine kawachukua jeshini, yarabi Mungu kaamua kuichukua roho ya mpangaji Sasa wenye nyumba na familia wameonekana kila sehemu wengine wamebeba magodoro, wanaelekea kwenye nyumba yao,na sasa wamejiapiza kuirudisha nyumba mikononi mwao
Kila watakaemkuta watamtolea dirishani, ndio maana NAPE kamwambia Polepole kina wenyewe shekhe! Polepole na wenzake hawaamini kama wanatakiwa kuwapisha wenye mji, mwendazake aliwapiga makufuli mpaka waasisi,mzee Makamba Kama hakuwepo, Kinana Kama hakuwepo,wengine ilibidi tu watangulie ili kumuondolea bugudha mpangaji 😂😂