Ng'ombe mkali

sultanwjps

Member
Joined
Jun 27, 2010
Posts
14
Reaction score
0
Kule kisiwani pemba mchezo wa n'gombe ni maarufu sana na kuna n'gombe wengi wakali
na wachezaji stadi.
any how kulikua na n'gombe mmoja mkali kupita wote kwa umaarufu anaitwa KIPOLE.
Sasa stori ni kua mtu mmoja wa makamo alikua akilima kwenye kajishamba kake na
ikafika wakati wa kusali , akajitayarisha kwa sala na akaanza kusali. sio mara akapita kijana mmoja anayemfahamu na akataka kuchokoza yule mzee anaesali na mambo yakawa kama hivi :

Kijana : akampigia kelele yule mzee anaesali "Binaami asalie hasemi lakini asikia
basi nakupa habari kipole kakata tena anakuja huku , huko nyuma keshaua
basi ni hiariyako kutataka sala yako au roho yako.

Yule mzee kusikia habari hii ya kutisha akaacha kusali na akaanza kukimbia mbio nyingi sana.

jioni siku ile yule kijana akakutana na yule mzee na akawambia Binaami kumbe wamuogopa KIPOLE zaidi kuliko Mungu wako. waacha sala yako kwa kumkimbia KIPOLE:smiling:
 
hahahaha kwenye hatari lazima utimue mbio huku unaomba mungu nisaidie mie mja wako
 
utasali vipi na hofu?

lazima ukimbie ................mungu utamuomba msamaha baadae
 
Kifo cha kupigwa au kushambuliwa na mnyama ni kibaya zaidi.baadaye unaweza kurudia toba yako na ikakubalika.inshaalah
 
usipokimbia mungu atakushangaa.............labbda kama na yeye akili zake kama za ngombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…