Ng'ombe wangu ana shida gani?

Ng'ombe wangu ana shida gani?

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Ng'ombe wangu aina ya Jersey kazaa leo hii. Amechoka sana ameshindwa hata kumlamba mwanaye kondo halijatoka msaada please.
 
Ng'ombe wangu aina ya Jersey kazaa leo hii. Amechoka sana ameshindwa hata kumlamba mwanaye kondo halijatoka msaada please
Kama nitakuwa sijachelewa, kwanza kuchoka kwake inamaana katumia nguvu nyingi katika kuzaa hivyo ungempa maji ya glucose ya kutosha.

Pili kutoa kondo ungempatia maji yenye chumvi inasaidia. Kwa ndama inatakiwa umpatie maziwa ya kwanza ya mama hata kwa kumkamua mwenyewe. Muhimu zaidi mtafute mtaalamu wa mifugo.
 
Hivi kuna ukweli eti ng'ombe akizaa kondo likitoka akalila maziwa yanatoka kidogo sana?
Kondo limetoka nikiwa sipo sijui limekwenda wapi labda mbwa wamekula maana nina.mbwa
 
Back
Top Bottom