Ngome ndogo ya von Wissman Bagamoyo

Ngome ndogo ya von Wissman Bagamoyo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NGOME NDOGO ALIYOJENGA HERMANN VON WISSMAN BAGAMOYO

Kiasi cha miaka 10 iliyopita nilifika kwenye hii ngome ndogo aliyojenga Hermann von Wissman wakati jeshi lake lenye askari wa Kinubi na Kizulu walipokuwa wanapambana na jeshi la Abushiri bin Salim Al Harith.

Wakati huo niliikuta ngome hii imesimama imara na kuna mlango na kwenye mlango wake kulikuwa na kibao cha maelezo ya historia hii ya kijumba hicho.

Mbele ya ngome hii kuna kaburi wenyeji wanasema amezikwa mmoja wa askari wa von Wissman jina lake Mgonela na kabila yake ilikuwa Msukuma.

Wakati ule sehemu hii yote kuzunguka ngome hii ilikuwa ni pori tupu na kazi ya Mgonela ilikuwa kupanda juu ya mnazi na kuangalia wapi majeshi ya Abushiri yanapotokea na kutoa taarifa.

Nyumba hii ina matundu ya kupitishia bunduki na kuangalia nje na humu ndani ndimo Wissman akiweka silaha za vita na risasi.

Hii nyumba leo haina mlango na imebomoka vibaya sana na si muda mrefu itatoweka yote pamoja na historia yake.

Watoto wa askari hawa wa Kinubi na Kizulu waliopigana chini ya von Wissman dhidi ya Abushiri walikuja kuwa watu mashuhuri katika mji wa Dar es Salaaam baada ya Wajerumani kuhamisha makao ya serikali kutoka Bagamoyo kwenda Dar es Salaam.

Historia ya Dar es Salaam ina mengi ya kuhadithia ya Affande Plantan na wanae Thomas Saudtz Plantan, Schneider Abdillah Plantan, Ramadhani Mashado Plantan na ndugu yao wa mbali Kleist Abdallah Sykes.

Baba zao walishiriki katika vita hivi Bagamoyo dhidi ya Abushiri wakitokea Pangani walikoletwa na manowari ya Kijerumani kutoka Laurenco Marques wakiwa wameongozana na von Wissman.

Baada ya kumshinda Abushiri na kumnyonga wakapelekwa Kalenga kwenda kupigana na Mtwa Mkwawa.

Ngome hii ni sehemu muhimu ya historia ya wazee wetu na inaeleza athari mbaya za ukoloni kuwa uliweza kuwatoa Waafrika Mozambique kuwaleta Ostafrika (Tanganyika) kuja kupigana na Waafrika wengine ili wakubali kutawaliwa na Wazungu.

Vita Vya Kwanza Vya Dunia vilipoanza watoto wa askari wale ambao baba zao walipigana Bagamoyo na Kalenga karne iliyopita na wao kama walivyokuwa baba zao askari katika jeshi la Wajerumani wakaingizwa vitani chini ya von Lettow Vorbeck kupigana na Waingereza kulinda himaya ya Wajerumani Tanganyika.

Kleist Sykes akiwa na miaka 17 na nduguye Schneider Plantan ndani ya jeshi la Wajerumani chini ya von Lettow Vorbeck wakitembea kwa miguu walipita kwa miguu Bagamoyo wakielekea Mwele Juu, Tanga kwenda kupambana na majeshi ya Kiingereza yaliyovuka mpaka na kuingia Tanganyika yakitokea Taveta.

Ukoloni haubadili rangi yake kwa haraka.

Vita Vya Pili Vya Dunia wajukuu wa askari hawa ambao vizazi vyao viwili viliingia vitani kuwahami Wajerumani dhidi ya Waingereza ndani ya Tanganyika, wajukuu wakajikuta wako katikati ya Bahari ya Hindi ndani ya meli zikisindikizwa na manowari za Kiingereza kuelekea Burma kupigana ndani ya King's African Rifles (KAR) dhidi ya majeshi ya Hitler na washirika.

Historia hii imebakia kwetu kwa kuwa na kumbukumbu kama hii ngome ya von Wissman iliyoko Bagamoyo ambayo si miaka mingi ijayo itakuwa imetoweka.

Picha: Abushiri na jengo la Hermann von Wissman.

Screenshot_20210908-112929_Facebook.jpg


Screenshot_20210908-113217_Facebook.jpg


Screenshot_20210908-113336_Facebook.jpg


Screenshot_20210908-113711_Facebook.jpg
 
Jumba hili ndio lile liitwalo ngome kongwe pale bagamoyo?
 
Siku moja nilitembelea majengo mengi ya bagamoyo. Nilikuwa na kijarida kinaelezea historia ya hayo majengo. Inafurahisha sana kujifunza historia yao. block house, arab coffee house, jumba la dhahabu, india street nk.
 
inakua vip nyunb yenye historia kama hio inaachwa inakufa hivo kwann pasiwekwe information center hapo na paka tunzwa pawe ni sehem yabutaliii
 
inakua vip nyunb yenye historia kama hio inaachwa inakufa hivo kwann pasiwekwe information center hapo na paka tunzwa pawe ni sehem yabutaliii
Umeshafika bagamoyo lakini?majengo ya aina hii ni mengi sana
 
Umeshafika bagamoyo lakini?majengo ya aina hii ni mengi sana
Mdukuzi,
Nimefika Bagamoyo mara nyingi.
Mmoja wa babu zangu Shariff Taib ni mwenyeji wa Bagamoyo.

Majengo mengi yamebomoka ni kweli lakini hili lina umuhimu wa pekee kwani lilijengwa na Hermann von Wissman aliyekwenda Kwa Likunyi, Imhambane, Mozambique kutafuta askari mamluki kuja German Ostafrika kupigana na Abushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa.

Historia ya Wazulu wale kutoka Mozambique nimeieleza hapa pamoja na athari zake katika historia ya Tanganyka.

Ngome hii ya Wissman ni moja ya vielelezo vinavyokamilisha historia ya wazee wangu.
 
Umeshafika bagamoyo lakini?majengo ya aina hii ni mengi sana
magof kuwa meng na yakawa yanaharibika hilo ji suala lingine ambalo linahitaji jicho la kipekee.huon miji ya roma au giriki inavopata miminiko la watalii kila mwaka just kwa kuyatunza majengo ya enzi na enz.
hiv unafikir bagamoyo ingepewa upendeleo maalum ikatolewa hhata paper ya wake up call kuyakarabat majengo yote yotee ungakua unaingiza kias gan watalii wa nje na na ndan?
hilo kamb la wissman hata ubalonz wangeombwa wangelipa tafu.si kuna institute wana hela hata wale goethe cultural
 
magof kuwa meng na yakawa yanaharibika hilo ji suala lingine ambalo linahitaji jicho la kipekee.huon miji ya roma au giriki inavopata miminiko la watalii kila mwaka just kwa kuyatunza majengo ya enzi na enz.
hiv unafikir bagamoyo ingepewa upendeleo maalum ikatolewa hhata paper ya wake up call kuyakarabat majengo yote yotee ungakua unaingiza kias gan watalii wa nje na na ndan?
hilo kamb la wissman hata ubalonz wangeombwa wangelipa tafu.si kuna institute wana hela hata wale goethe cultural
Uko sahihi kabisa ila Kikwete namlaumu sana yeye ndiye alitakiwa kuifanya bagamoyo kuwa kitovu cha utalii lakini wapi,uwezo huo alikuwa nao,yale magofu yanatakiwa kutengewa bajeti ya kuyanusuru
 
Back
Top Bottom