"Ngome ya Vijana ACT Wazalendo tunalaani vikali ukatili na unyama huu unaofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya Raia wanaotumia haki na uhuru wao wa kufuatilia kesi Mahakamani kwa amani na utulivu. Hili ni shambulio kubwa dhidi ya haki, Demokrasia na uhuru wetu. Hatuwezi kukubali nchi yetu Tanzania kugeuzwa kuwa nchi ya ubabe na upolisi (Police State)."