Ngono kwa kupitia mdomo inasababisha Saratani

Ngono kwa kupitia mdomo inasababisha Saratani

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
mdomo.jpg

Mdomo ukliwa umeathiriwa na bakteria kufuatia kutumiwa kama njia ya kufanya mapenzi

Saratani imeendelea kuwa tishio hapa nchini huku hofu ikiendelea kuikumba jamii kutokana na wataalamu wa afya kushindwa kufahamu tiba halisi ya maradhi hayo hatari.
Takwimu kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha ongezeko la saratani ya mdomo na koo kwa kiasi kikubwa kutoka kesi 167 mwaka 2006 hadi 277 mwaka 2012. Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Ocean road, Julius Mwaiselage anaeleza kuwa watanzania wasipende kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo. "Saratani ya mdomo ipo, na nyingine zinasababishwa na zinaa " anasema Dk Mwaiselage

Tafiti za saratani
Tafiti mbalimbali zimewahi kufanyika nchini na kubaini kuwepo kwa ongezeko la saratani ya mdomo.Utafiti uliofanywa na Dk Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), umebaini aina za saratani 1,594, kati ya hizo 509 zikiwa ni za midomo kwa mwaka 2003 pekee.
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa kati ya saratani 509 za mdomo, saratani 242 zilisababishwa na Virusi vya Human Papiloma ambavyo hutokana na zinaa. "Ninachojua mimi ni kuwa Virusi vya HPV husababishwa na magonjwa ya zinaa, hivyo mtu anayeugua saratani ya aina hiyo, imetokana na zinaa," anasema Dk Mosha.

Wanaume waathirika zaidi wa Saratani
Takwimu hizo ni zile zilizopatikana kwa watu waliokwenda kufanyiwa uchunguzi katika Mkoa wa Dar es Salaam pekee.
Dk Mosha anasema kuwa wanaume ndiyo huathiriwa zaidi na saratani ya mdomo ambapo kwa hapa nchini, asilimia 53 ya wanaume waliofika MNH kwa ajili ya vipimo, walibainika kuugua saratani hiyo, huku wanawake wakiwa ni asilimia 47. Utafiti kama huo ulifanywa pia na Dk Amos Mwakigonja, mkuu wa Idara ya Patholojia katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MUHAS).

Dk Mwakigonja alifanya utafiti wa saratani ya mdomo aina ya Kaposi's Sarcoma ambapo wagonjwa 78 walibainika na saratani hiyo kuanzia mwaka 1990 hadi 2003. "Saratani za mdomo zipo za aina nyingi na zimetofautiana kulingana na visababishi vyake," anasema Dk Mwakigonja. Katika utafiti wake Dk Mwakigonja alibaini kuwa wanawake wengi walikuwa na saratani ya mdomo aina ya Kaposi's Sarcoma kuliko wanaume.

Hata hivyo, utafiti huo ulionyesha kuwa asilimia 50 ya wanaume walikuwa na saratani ya mdomo hatari zaidi (systemic) kuliko wanawake ambao ni asilimia 37.

Mapenzi kwa mdomo husababisha maradhi
Dk Mwakigonja anasema kuwa mapenzi yoyote kwa njia ya mdomo lazima yasababishe maradhi ya zinaa iwapo mmoja ameambukizwa. Pia anasema kwamba sampuli nyingi za wanaume wanaojihusisha na mapenzi na wanaume wenzao (mashoga) zilibainika na saratani ya mdomo. Utafiti huo ni sehemu ya utafiti wa Shahada ya Uzamivu ambao ulionyesha kuwa wagonjwa wengi wa saratani ya mdomo walikuwa ni wanaume wenye umri wa miaka kati ya 38 na kuendelea na wanawake ni 31.

Ufatiti wa WHO Tanzania
Shirika la Afya Duniani (WHO) pia lilifanya utafiti mwaka 2010 nchini kwa kushirikiana na Kituo cha Taarifa za HPV, ambapo ilibainika kuwa asilimia 20 ya saratani za koo na mdomo nchini zinasababishwa na ufanyaji wa mapenzi kwa njia ya mdomo.

Taarifa hizo za WHO zinaeleza kuwa wanaume 747 hugundulika na saratani ya mdomo kila mwaka wakati wanawake 472 hubainika na saratani hiyo pia.
Wakati huohuo, wanaume wanaopoteza maisha kutokana na saratani hiyo ni 444, kwa mwaka na wanawake ni 270, kwa mwaka. Utafiti wa WHO umebaini kuwa saratani ya mdomo inashika nafasi ya sita katika aina 24 za saratani 24 zinazoisumbua zaidi Tanzania.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa wanaume wanaoathirika zaidi ni wenye umri wa kati ya miaka 15 na 55, ambao tayari wameshaanza kujihusisha na ngono.
Kama maradhi mengine ya kuambukiza, Virusi vya HPV huambukizwa kwa urahisi zaidi kutoka kwa wanawake kwenda kwa wanaume kuliko kutoka kwa wanaume kwenda kwa wanawake. Utafiti huo uliodhaminiwa na mfuko wa Bill na Melinda Gates na Kituo cha Saratani na Mpango wa Utafiti wa Taasisi ya ICO unaeleza kuwa mitandao ya kijamii na picha za ngono ndiyo chanzo cha watu wengi kuiga ufanyaji wa mapenzi ya aina hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la The New York Times, tafiti zimefanyika na kubaini kuwa asilimia 70 ya wagonjwa wanaobainika na saratani ya koo na mdomo duniani, husababishwa na Virusi vya Human Pappiloma vinavyotokana na magonjwa ya zinaa.Tafiti hizo zinaonyesha kuwa wagonjwa wengi wanaogundulika na saratani hiyo ni wanaume wenye umri wa kati, wenye uwezo wa kifedha, wasiovuta sigara wala siyo walevi waliokubuhu.

Utafiti huo ulibaini kuwa wanaume wapo hatarini zaidi kupata saratani ya koo inayosababishwa na Virusi vya HPV. Miaka ya 80, idadi ndogo ya watu waliougua saratani ya koo walihusishwa na maambukizi ya Virusi vya HPV. Kihistoria, watu waliobainika na ugonjwa huo, ni wenye umri wa miaka 70 kwenda juu ambao walikuwa ni wale walevi waliokubuhu na wavuta sigara.

Ilielezwa kuwa Virusi vya HPV vipo kwa wingi kiasi ambacho watu wazima wanaojihusisha na ngono ya aina yeyote ile, huweza kupata maambukizi ya zinaa hata kama siyo saratani. Hata hivyo ilibainishwa kuwa saratani isababishwayo na virusi vya HPV ni rahisi kuitibu kuliko saratani ya koo isababishwayo na tumbaku au pombe kali.

Virusi vya HPV ni nini?
Kwa jina la jumla, saratani ya koo au mdomo huitwa saratani ya kichwa na shingo. (Neck and Head Cancer) HPV ni miongoni mwa virusi hatari zaidi duniani visababishwavyo na magonjwa ya zinaa na vinaweza kuathiri sehemu mbalimbali za mwili. Zipo aina zaidi ya 120 za HPV, baadhi huweza kuzalisha usugu (warts) ambazo si saratani katika sehemu za siri, mikononi na miguuni. Maambukizi ya HPV hufanyika kwa urahisi, hata kwa kugusana ngozi au majimaji, huku maambukizi mengine yakisababishwa na ngono.

Virusi hatari na vinavyosababisha saratani ni HPV-16, HPV-18, HPV-31 na HPV 45. Aina hii ya Virusi vya HPV husababisha saratani ambapo uvimbe waweza kujitokeza kwa ndani na unaweza usionekane ukilinganisha na vivimbe vingine vya saratani. Wataalamu wanasema HPV-16 na HPV-18 inahusishwa zaidi na saratani ya shingo ya kizazi na endapo mapenzi kwa njia ya mdomo yatafanywa na mtu mwenye uambukizo huu ni rahisi kuambukizwa.

June, 2013

--------------------------------------------




Leo ni siku ya Saratani Duniani. Wakati tunaadhimisha siku hii hapa nchini idadi ya vijana ambao ni tegemeo la taifa inazidi kupungua kutokana kuangamia kwa saratani ikiwemo ya koo. Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex".


Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili, pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi. Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.

Katika utafiti huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747 na wanawake wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo. Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni kuwavutia wapenzi wao katika kushiriki ngono. Vijana wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo. Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani ya koo ni ya pili katika mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume nchini, ikiongozwa na ile ya ngozi (Karposi's Sarcoma) ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua Tanzania. Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya watu hupata saratani ya koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine kuwa na umri mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.

"Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya wanawake inatokana na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume ili aweze kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili hii haikuwepo kabisa," anasema Dk Kahesa na kuongeza. "Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila kujua madhara yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,"anaongeza

Sababu nyingine zaidi
Anasema staili ya maisha nayo imechangia kuongezeka kwa ugonjwa huo, vijana wengi kwa sasa hutumia muda mwingi kuangalia video za ngono na staili zinazofanywa na wenzetu wa nje na hivyo kuongezeka kwa matumizi ya ngono ya mdomo. Dk Kahesa anasema asilimia 12 ya wagonjwa wote wa saratani nchini wanasumbuliwa na saratani ya koo, hivyo kuna kila sababu kwa vijana kubadilisha tabia na kuepuka kuiga mitindo ya wenzetu wazungu ambayo mara nyingi inapotosha mila na tamaduni za Kiafrika.


Anasema katika mtiririko wa saratani zinazoongoza nchini saratani ya koo inashika nafasi ya tano, wagonjwa wengi wanaopatwa na ugonjwa huo ni watu wenye umri mkubwa wa miaka 60 na kuendelea hiyo inaonyesha kuwa wengi wao walianza ngono ya mdomo muda mrefu wakati wakiwa bado wadogo. "Asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopatikana na kansa ya koo nchini, inawapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea kutokana na wengi wao kuanza mapema vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo wakati bado wadogo au wengine kurithi kutoka kwa wazazi wao," anasema Dk Kahesa.

Aina ya kansa ya koo
Tafiti zinaonyesha kuna aina mbili za saratani ya koo; aina ya kwanza ni "Oesophagus Carcinoma na Squamous cell carcinoma, zote hutofautiana wakati zinapimwa kwenye darubini lakini matibabu yake yanafanana. Aina hizo ndizo zilizopo nchini na huanza mapema kuharibu seli ambazo zipo katika utandu uliopo katika ukuta wa koo kabla ya kuenea katika maeneo mengine ya koo.


Visababishi vya kansa ya koo:
Moja kati ya vitu vinavyosababisha kansa ya koo ni mwenendo wa maisha yetu kwa kula vyakula vyenye asidi, vyakula vichachu, vyakula vyenye pilipili, pombe kali na vyakula vigumu ambavyo hukwaruza koo na hivyo kusababisha saratani. Anasema asilimia 90 ya wagonjwa wanaopokelewa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean road wanakuwa na historia ya kutumia vikali kama pombe kali, kuvuta sigara kwa kupindukia, kula pilipili kwa wingi na kutumia vitu vyenye uchachu.


Dalili za saratani ya koo
Moja kati ya dalili za mgonjwa wa saratani ni chakula kukwama kwenye koo, siku za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa kumeza chakula kigumu kisha cha majimaji na baadaye akashindwa kumeza hata mate. Ugonjwa huo unachukua muda mrefu kugundua na kuona viashiria kwani mwanzo mgonjwa huanza kupata shida kumeza chakula na kwamba wagonjwa wengi wanaofika katika Taasisi hiyo ya Saratani wanakuwa tayari wamechelewa kwani wanakuwa katika hatua ya mwisho.


"Unaweza usionyeshe dalili lakini kadri siku zinavyokwenda ndiyo kunakuwa na dalili zinajitokeza pia katika kipindi hicho mtu anakuwa na maumivu wakati wa kumeza chakula, maumivu katika kifua na mgongo na hata kupungua uzito pamoja na kikohozi kikavu kinachoweza kudumu mwezi mmoja," anasema.

Njia ya kuzuia saratani ya koo.
Kwanza mtu mwenye ugonjwa huo anapaswa kuhawi hospitali ili aanze matibabu mapema kutokana na ukweli kwamba mgonjwa anayewahi kupata matibabu ana uwezekano wa kupona kuliko yule ambaye amechelewa kugundulika na kuanza matibabu. Kama saratani hiyo itakuwa imeshambulia viungo vyote vilivyopo jirani na koo na hadi kufika katika tezi au kiungo kingine cha mwili, mgonjwa anaweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji, kutumia mionzi na hata kifaa maalumu ambacho ni kemikali.


Tafiti zilizofanywa nchini
Wataalamu mbalimbali nchi wamefanya tafiti zinazohusiana na ugonjwa huo na kusema kuwa kati ya mwaka 1983 hadi 1992 kulikuwa na kati ya watu 546 waliopimwa, wanaume 430 na wanawake 116 waligundulika kuwa na ugonjwa huo. Utafiti huo ulishirikisha watu wenye umri wa miaka 21 hadi 90, ulibaini kuwa wagonjwa wengi walikuwa wenye umri wa miaka 50-59 tofauti na hali iliyopo sasa ugonjwa wa kansa ya koo unawaathiri vijana wenye umri wa miaka 40.


Dk Kahesa anasema katika kipindi cha miaka saba iliyopita takwimu za taasisi yake imeongezeka kutoka kutoka wagonjwa 167 hadi kufikia wagojwa 277. Hali inaonekana huenda ikaongezeka kutokana na ukweli kwamba wengi wa watu wanaonekana kuendeleza tabia hatarishi zikiwemo hizo za kutumia midomo.

Magonjwa mengine sehemu za siri
Miongoni mwa magojwa ambayo yanaweza kumpata mtu ambaye ananyonya au kulambana sehemu hizo ni pamoja na gonjwa wa gonoreha, ambapo ugonjwa huu huanzia katika koo na mwanzoni huhisi kama ni ukavu wa kifua au maradhi ya kawaida ya kifua, ila baadaye hushuka na kuelekea katika viungo vya uzazi.


  • Ugonjwa mwingine ni kaswende ambao huambukizwa kirahisi zaidi kupitia mdomo na hasa pale inapotekoa mdomo unapokutana na kiungo chenye athari hizo.
  • Vile vile ugonjwa wa chlamydia ni moja wapo kati ya magonjwa ya zinaa ambao huambukizwa kwa bakteria na kwamba ugonjwa huu pia huambukizwa kupitia mdomo, ingawa waathirika wanaweza wasijijue maana huwa hauna dalili kwa muda mrefu.
  • Hepatitis A: Hiki ni ni kirusi kinachopatikana katika kinyesi cha binadamu, kirusi hiki huwaingia wale wanaopenda kunyonya na kulambana sehemu za haja kubwa. Ni kwamba kwa ugonjwa huu mtu anaweza akaharibika macho hadi kupofuka.
  • Hepatitis B: Ugonjwa huu huambukizwa kama virusi vya Ukimwi kwa sababu virusi vyake hukaa katika majimaji yanayotoka katika sehemu za siri na damu. Mtu akiwa na ugonjwa huu, mwili wake unakuwa na vipele vingi na hata majipu ambayo huwa magumu kupona na wapo wanaokufa.
  • Vile vile ugonjwa wa Hepatitis C: ni ugonjwa ambao hupatikana pindi damu inapotoka maana vijidudu vyake vinakaa katika damu. Ugonjwa huu humfanya mtu kuvimba viungo na hata kukatika.
  • Hata hivyo kupitia staili hii yaupeana raha kwa kunyonyana sehemu za siri, kuna uwezekano wa kupata maambukiz ya virusi vya Ukimwi kwa uchache lakini kwa nchi zilizoendelea wamebuni aina ya kondom ambazo huvaliwa katika mdomo wa binadamu na hivyo kupunguza hatari ya kupata madhara hayo.

JE NGUVU ZA KIUME ZINACHANGIA?
Dk Kahesa anasema hakuna utafiti wa moja kwa moja unao onyesha kuwa baadhi ya wanaume wanaofanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na upungufu wa nguvu za kiume.

"Utafiti wa mtu mmoja hautoshi kuonyesha kuwa baadhi ya wanaume wanafanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na ukosefu wa nguvu za kiume, hivyo kinachotakiwa ni kufanya utafiti wa kina ili kubaini kama tatizo hilo lipo licha ya kuwepo kwa kesi nyingi zinazodaiwa kuwa baadhi ya wanaume hawana nguvu za kiume na wapenzi wao huwafichia siri kwa kufanya nao mapenzi kwa njia yam domo"anasema.

NINI KIFANYIKE:
Wataalamu wa masuala ya ndoa na saikolojia wanasema kuna njia nyingi za kuandaana wakati wa tendo la ndoa tofauti na kunyonyanyana sehemu za siri. Wataalamu hao wanasema sio sahihi kwa mwanaume au mwanamke kunyonyana sehemu za ndoa mwenzake na kwamba staili hizo ni staili za wanzetu wa nje lakini kitu kinachosababisha kukua kwa kasi kwa staili hiyo ya kunyonyonyana sehemu za siri au kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ni kutokana na kasi ya utandawazi.


Wadadisi wa mambo wanadai kuwa baadhi ya watu huiga staili hizo kutoka katika mitandao bila kujali kuwa kuna zina madhara makubwa, hivyo ni jukumu la kila mtu kulinda afya yake na ya mwenza wake.

Sio kila kitu kinachowekwa katika mitandao ya kijamii kina manufaa la hashaa! vitu vingine vinachangia kuhatarisha maisha.


February, 2014
 
Hebu fafanua , unaposema ngono kwa mdomo unamaanisha nini?.

Kuna njia nyingi ambazo watu hufanya mahusiano kwa njia zisizo za kawaida mojawapo ikiwa ni lips, ulimi, vinywa nk. Kwa kufanya hivyo ni dhahiri virusi vya magonjwa kutoka mwa mmoja husambaa kwa mwingine kwa vile kwa kufanya hivyo hupakana vijidudu vya maradhi kirahisi na kwa hakika zaidi.
 
Njia ya kawaida ndio ipi?

Kawaida kwa nani?

Jambo la msingi ufafanuzi wa kitaalamu pamoja na maelezo yake soma mada inayotolea ufafanuzi juu ya hilo ambapo wataalamu wametafiti juu ya hilo. Ujembe umefika, na kwa kawaida mjumbe hauawi.
 
Jambo la msingi ufafanuzi wa kitaalamu pamoja na maelezo yake soma mada inayotolea ufafanuzi juu ya hilo ambapo wataalamu wametafiti juu ya hilo. Ujembe umefika, na kwa kawaida mjumbe hauawi.

Ufafanuzi wa kitaalamu haujataja "njia za kawaida"

Dhana hiyo umeileta wewe

Tueleze ndio zipi?
 
Ufafanuzi wa kitaalamu haujataja "njia za kawaida"

Dhana hiyo umeileta wewe

Tueleze ndio zipi?

Kama unataka darasa niambie, kama ni ubishi achana nayo we endelea na mazoea yako, na wanaotaka kuwa na tahadhari huu ni ujumbe muhimu kwao. Hata katika familia kuna watoto wasikivu na kuna wasioambilika, kwa maana hiyo hatushangai wengine kutoguswa na hivyo kuibua ubishi wakati wengi wanaambukizwa magonjwa kwa njia hiyo.

Fikiria kulambana ndimi au kunyonyana midomo ni jambo ambalo wahusika hubadilishana mate na majimaji toka kwa mwenzake wakati mate na majimaji hayo kwa baadhi yamejaa virus hatari wa magonjwa, sisi tunachangamkia tu ndio mahusiano ya kileo.
 
Kama unataka darasa niambie, kama ni ubishi achana nayo we endelea na mazoea yako, na wanaotaka kuwa na tahadhari huu ni ujumbe muhimu kwao. Hata katika familia kuna watoto wasikivu na kuna wasioambilika, kwa maana hiyo hatushangai wengine kutoguswa na hivyo kuibua ubishi wakati wengi wanaambukizwa magonjwa kwa njia hiyo.

Fikiria kulambana ndimi au kunyonyana midomo ni jambo ambalo wahusika hubadilishana mate na majimaji toka kwa mwenzake wakati mate na majimaji hayo kwa baadhi yamejaa virus hatari wa magonjwa, sisi tunachangamkia tu ndio mahusiano ya kileo.

Nataka darasa
 
Huwa nafurahi mtu akitoa maelezo mengi na yaliyojitosheleza kuhusu mada husika! Mia!
 
Kuna njia nyingi ambazo watu hufanya mahusiano kwa njia zisizo za kawaida mojawapo ikiwa ni lips, ulimi, vinywa nk. Kwa kufanya hivyo ni dhahiri virusi vya magonjwa kutoka mwa mmoja husambaa kwa mwingine kwa vile kwa kufanya hivyo hupakana vijidudu vya maradhi kirahisi na kwa hakika zaidi.

kama nimekusoma vizuri, unamaanisha viungo vya siri (genital organs) havitakiwi kugusana na mdomo kama vile kunyonya sehemu za siri kwa mdomo, am i right?. but romance is ok, isnt it? .Thanx
 
Kunyonya nanii ya mwenzio!!

Thanx mkuu nimekusoma, unajua haya mambo yanatakiwa kuwekwa wazi ili vijana wajifunze.siku hizi kuna watu esp.vijana bila kunyonyana ikulu wanaona hajafanya kitu.
 
Kama unataka darasa niambie, kama ni ubishi achana nayo we endelea na mazoea yako, na wanaotaka kuwa na tahadhari huu ni ujumbe muhimu kwao. Hata katika familia kuna watoto wasikivu na kuna wasioambilika, kwa maana hiyo hatushangai wengine kutoguswa na hivyo kuibua ubishi wakati wengi wanaambukizwa magonjwa kwa njia hiyo.

Fikiria kulambana ndimi au kunyonyana midomo ni jambo ambalo wahusika hubadilishana mate na majimaji toka kwa mwenzake wakati mate na majimaji hayo kwa baadhi yamejaa virus hatari wa magonjwa, sisi tunachangamkia tu ndio mahusiano ya kileo.

Asante mkuu. Message sent.
 
kama nimekusoma vizuri, unamaanisha viungo vya siri (genital organs) havitakiwi kugusana na mdomo kama vile kunyonya sehemu za siri kwa mdomo, am i right?. but romance is ok, isnt it? .Thanx

429996_200694123417827_432136077_n.jpg


Kumbuka kimaumbile sehemu za viungo vya uzazi kuna tindikali ambayo husaidia kuua vijidudu tofauti na ilivyo kwa viungo vya kuongelea na kulia vyakula (mouth, lips & tongue) ambavyo tindikali haiko mdomoni zaidi ila tumboni ambako chakula kinafikia kwa ajili ya process. Ndio maana hata mtoto anapozaliwa kuna tahadhari sana kutocheleweshwa wakati wa kuzaliwa kama mfuko wa uzazi umeshapasuka ili asinywe maji ya tingikali yakamtoa uhai.
 
Mwali haya mambo yasipofafanuliwa vizuri yanachanganya sana!
RISK ya saratani ipo kama mnyonywaji ana magonjwa ya zinaa
1. sio kila magonjwa
2. sio kila myonywaji atakua na magonjwa
3. hata akiwa na magonjwa, sio lazima saratani itokee!
Oral sex is not the risk, magonjwa ya zinaa are.
Kabla ya sex pimeni! this is the main idea!
 
RISK ya saratani ipo kama mnyonywaji ana magonjwa ya zinaa
1. sio kila magonjwa
2. sio kila myonywaji atakua na magonjwa
3. hata akiwa na magonjwa, sio lazima saratani itokee!
Oral sex is not the risk, magonjwa ya zinaa are.
Kabla ya sex pimeni! this is the main idea!


wiki hii hii scaremongering ilivyo tanda
sijui kama kuna watu wata thubutu lol
 
Back
Top Bottom