SoC02 Ngono na mazao ni biashara ya kubadilishana, yaani batter trade ya vijijini hivi sasa

SoC02 Ngono na mazao ni biashara ya kubadilishana, yaani batter trade ya vijijini hivi sasa

Stories of Change - 2022 Competition

Rangi ya chai

Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
7
Reaction score
9
Kuna wimbi kubwa ya biashara haramu ya ngono vijijini hivi sasa. Biashara hii ni mpya kabisa kutokea sio kama inayofanyika mjini.

Wadada wanakuja vijijini ,hasa wakati wa mavuno ,wanaweka kambi kwa kupanga vyumba hivi hivi vya tembe. Kisha wanaanza biashara ya kubadilisha .

Iko hivi ,kule mijini ni mwanaume anatoa pesa Kisha anapewa huduma ya ngono kwa mishindo atakayo kwenda.

Lakini huku vijijini wadada wanataka mazao Yani wanaume wanapeleka mazao wala hata hayadhaminishwi na Bei ya kipindi hicho ,mfano unaweza kuwa mashindo moja kwa debe la mahindi, mpunga au choroko.

Wadada hao wanatoka sehemu mbalimbali ya nchi ,wanakusanya mazao hayo wanajaza kwenye magunia. Kisha wanapotosheka wanakodi magari ya kusomba na Kisha kutoweka ili kusubiri msimu mpya.

Hii inaweza kusababisha balaa la njaa na umaskini katika jamii na familia za waishio vijijini.
Na pia Haina afya kwa ustawi wa familia kwani wahanga ni wanawake na watoto wanashiriki katika kilimo na Kisha wanahujumiwa na waume zao kwa kutumia mazao kwa ajili ya kupata huduma ya ngono . Taasisi za haki za wanawake pazeni sauti katika hili sio mnajikita mijini pekee na vijijini pia Kuna wanawake wenzenu.

Biashara hii imekithiri Sana maeneo ya Shinyanga vijijini ,kishapu na maeneo ya jirani yenye shughuli za kilimo.

Kwa mtazamo wangu biashara ya namna hii ikomeshwe kwa sababu inadumaza uchumi wa vijijini na familia nyingi.
Kwani wakishakusanya wanatoweka na kwenda kunufaisha kwingine.
 
Upvote 9
Ndo vizuri watu wapate Hamasa ya kukwatua vizuri sababu unajua ukitupia mbegu vizuri msimu wa mavuno unamwagilia pazuri
 
hii nchi mimi sijawahi kuona
nimecheka sana

hiyo ndo fursa
 
Nikiwa na sado iliyojaa michembe maelewano yako vipi....
 
hii nchi mimi sijawahi kuona
nimecheka sana

hiyo ndo fursa
Amini ndo iko Ivo bro, tulikofikia sasa hata mimi nabaki mdomo wazi. Shinyanga vijijini na kishapu karibu ujionee. #utalii wa ndani
 
Back
Top Bottom