CHE_BUEVARA
Member
- Aug 11, 2021
- 5
- 3
“Saa saba juu ya alama saa nikiitazama, nimeshaachana na Jackie sasa namfata salama, saa kumi na mbili nina appointment na mademu Wawili, achana na lily ambae tutakutana saa mbili.”
Hapo sasa Ferooz alikua anatusimulia namna ambavyo alikua anakula bata tena lile la kipindi cha miaka ya elfu mbili (2000) lilikua la watu wachache mnoo sio hili la siku hizi kila sehemu kuna kiwanja.
Bwana Mdogo akaendelea akisema “Starehe mimi nilizifanyia papara, nilibadili mademu kama vidaladala…” Lakini wakati huo anampanda huyu na kesho yule Ferooz alisema wala hakua anatumia kondomu kwamba itapunguza ladha ya tendo, utamu huu jamani! Hahaha
Ferooz alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuwafikishia ujumbe walengwa na hata baadhi ya dalili za ugonjwa alizotaja kwenye ule wimbo (starehe) zikawa ndio kipimo mtaani huku kujua kama mtu ana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ama lah.
The heavyweight MC akatubariki na mistari yake pale mizito kabisa ila ngoja tunukuu mmoja tuu, alisema “Starehe mnazipenda ila mwisho wake mbaya, wengi wameteketea kwa kuendekeza umalaya…” Basi kama daktari, Profesa akamshauri nini cha kufanya bwana mpenda chini ili aendelee kuishi.
Kwahiyo lile goma lilikua linatueleza ni vitu gani vinakuweka hatarini Zaidi kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi na humo humo tukapewa na namna gani tufanye kuepuka kuwa mhanga wa tatizo hili kubwa ambalo siku hizi watu kama wamelizoea hivi kiasi kwamba kuna hawa madogo ‘Mabantu’ wamesema eti kutumia kondomu kunapunguza utamu, unaona sasa vijana walivyo wa hovyo? “Niaje madam kama unanipa we nipe sijakataa UKIMWI upo ila kondomu inapunguza utamu.”
Sasa tujiulize, wangapi wanaruka na Asha kesho Mwanaisha jioni yake Amina hajaacha kuruka na Jesca hapo halafu hiyo miruko yote huenda hajavaa kinga kabisa au hata kuiwaza tuu hajawahi. Maana siku hizi unakuta goli la kwanza mtu anavaa halafu Sijui kinawapataga nini wanetu hawa, cha pili na kuendelea ni kiguu na njia yaani peku peku. Watu wanahisi kama UKIMWI umepoteza ubora wake hivi aisee dah! Ila ngoja tuendelee.
Maji muhimu sana, umekunywa ya kutosha? Fanya unywe maji bwana, mwili unayahitaji sana hayo.
Juzi kati hapo nilikua na wanangu tunapumzikiana na stori kumi uongo noja ya kweli, jamaa akasema siku hizi UKIMWI hamna kabisa kitaa, sasa cheki mazungumzo yetu yalivyokua
JAMAA: Siku hizi huo UKIMWI hamna kabisa kitaa
MIMI: Kwanini mzee?
JAMAA: Amini kwamba kaka, ujue zamani ilikua dude linatisha kinoma. Mtaani huku lazima utapishana na mtu kachoka mbaya, kakonda kama mtoto njiti vile
JAMAA: Ndo maana unaona wametuletea ugonjwa mwingine sahizi baada ya kuona hatufi yani (akimaanisha COVID-19)
Basi bwana,mtaani hawapendi mambo mengi nikamuuliza unaijua historia ya UKIMWI? Jamaa akaniambia vile anaujua tangu unaitwa Juliana, umeme, ngoma, ngwengwe, mdudu hadi sahizi unaitwa chai. Hahaha! Nikamuuliza kwanini unaitwa chai au ndio kuufanya uwe mwepesi tuu, akasema chai ni ya moto na inaunguza. Nikakosa pozi, tukaendelea na mambo mengine
Nilichokiona ni kwamba, watu wengi tunakomaa na matokeo na kuacha mchakato mzima wa kupata hayo matokeo tunayotarajia. Utakubaliana na mimi kwamba zamani ilikua ukienda kupima maambukizi haya na ikatokea umekutwa tayari wewe ni muathirika basi watasubiri hadi kinga mwili zishuke kwa kiasi Fulani ndio waanze kukupa dawa za kufubaza virusi na ndio hapo walipoteketea watu wengi mnoo.
Yani ugonjwa hauna tiba ila walikua wanasubiri uumwe ndio wakutibu, Hahaha! Dah! Akili hizi jamani.
Baadae wataalamu wakaona ile njia haifai, chap chap wakabadili mfumo, ukikutwa na virusi tuu siku hiyo hiyo unapewa ushauri ya namna ya kutumia dawa zako vizuri na ndio sababu hii siku hizi kumkuta mtu kakonda kisa VVU haipo yaani siku hizi waathirika wengi hawafiki hatua ya kupata ugonjwa wa UKIMWI, Sijui kama unajua kuna kuishi na Virusi vya Ukimwi na kuwa mgonjwa wa UKIMWI. Utakua unajua ila kuna wana wengi sana hawaijui hiyo kitu aisee.
Sasa kilichonichosha ni pale nilipoona ‘UNAIDS’ wametoa takwimu zao za kuongezeka kwa maambukizi ya VVU hasa kwa hawa ndugu zetu wa kike.
Unajua bwana mifumo ni jambo Fulani hivi gumu mno kwasababu watunga sera ni wengine, watendaji ni wengine na wahanga pia ni watu wengine wenye dunia yao nyingine kabisa. Hapo lazima ugumu uwepo kuyafikia yale malengo ya 90-90-90 hadi kufikia mwaka 2030. Hivi ni 90-90-90 au 95-95-95? Ujue haya mambo ya takwimu bwana yana wenyewe.
Mimi ni mnazi wa kuanzia chini siku zote kwasababu naamini ukimkunja samaki angali mbichi ndio utapata matokeo, haya matamasha na kampeni za kuleta uelewa wa masuala ya elimu ya afya ya uzazi tunawapa watu ambao washakauka. Si kwamba tuache kukesha na vijana hao wa miaka ya 25 na kuendelea, la hasha! Tuwekeze nguvu nyingi Zaidi kwa wadogo zao sasa ambao hata topic ya ‘Reproduction’ hawajaanza kuisoma.
Ni ngumu sana kumwambia paka wa zile Baa za mabibo pale kwamba maziwa fresh ndio chakula kitamu kuliko ile mifupa anayopewa kila siku baada ya watu kula nyama.
Kuna msemo unasema huwezi kupotea kama hujui unapokwenda sasa na hapa tunasema huwezi sema kondomu inapunguza utamu kama hukuanza kuonja bila kuitumia hiyo kondomu.
Halafu kabla sijaondoka hapa nakumbuka jinsi watu wanavyopenda kutishiwa ili wasifanye jambo Fulani, hebu tufikirie njia moja ya kuwatisha watu kama wakina Mabantu waache kufanya ngono zembe maana sasa dah! Mimi natumia kinga tena napenda zile zenye harufu ya strawberry na nina mpenzi mmoja mwaminifu, Mama Che Buevara. Hahaha! TUISHI [emoji1307]

Upvote
2