Ngono; sifa mpya inayotawala vyuo

British economist

Senior Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
104
Reaction score
14
[h=1]Ngono; sifa mpya inayotawala vyuo[/h] Hali kwa ujumla ni mbaya hasa katika baadhi ya vyuo. Rushwa ya ngono iko juu mno kiasi cha kukatisha tamaa. Mwalimu akimtaka mwanafunzi na akakataa, basi mwanafunzi huyo ajue kwamba ataambulia kufelishwa katika mitihani yake.
Viongozi na vyeti feki

Ingawa hakuna ushahidi lakini iko haja ya kuvitafiti vyeti vya viongozi wote katika ngazi zote, hii inatokana na hali ilivyoonekana huko Nigeria.

Licha ya Nigeria kuwa na vyuo vikuu kamili 73 na shirikishi zaidi ya 20, majenerali wasio na shahada wametawala taifa hilo muda mrefu!

Utafiti uliofanywa Nigeria mwaka 2005/06 na Benki ya Dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) ulibanisha kwamba mfumo wa elimu unadorora kwa kasi kutokana na rushwa.

“Nigeria ni taifa lililokuwa linazalisha wahitimu wa vyuo vikuu wenye hadhi ya kimataifa ambao waliweza kushindana na wahitimu wengine duniani.

Leo hii, tunazalisha wahitimu wa hovyo wasioweza hata kuumba sentensi rahisi,” anasema Dk. Roy Chikwem, Mnigeria msomi anayeishi Marekani.

Rushwa na udanganyifu katika elimu huko Nigeria vilipaa hadi spika wa zamani wa Bunge la Wawakilishi alipogundulika kuwa ameghushi cheti kuonyesha kuwa ni mhitimu wa Shahada ya Chuo Kikuu cha Toronto, Canada.

Hatimaye alilazimika kujiuzulu baada ya kashfa hiyo kufumuliwa na vyombo vya habari. Hata hivyo bado spika huyo aliendelea kuwa mwajiriwa wa Serikali. “Aibu gani?” anahoji Dk Chikwem.

“Cha kusikitisha zaidi,” anasema Dk Chikwem, “Ni ukweli kwamba wazazi wengi huamua kuwanunulia watoto wao nafasi za kujiunga vyuoni badala ya kuwahimiza ili wajitahidi kufaulu mitihani.

“Na kwa wazazi wanaokwepa kujiingiza katika uvunjaji huu wa maadili na sheria, matokeo yake ni kuwa waathirika kwani watoto wao hukosa kuendelea na masomo na kubaki nyumbani hadi wazazi wao wajue jinsi ya kulaghai mfumo uliopo”.

Dk. Chikwem anasema hatimaye wazazi hao huishia kutumia ule usemi maarufu wa Kiingereza: “If you can’t beat them, then join them”. Tafsiri yake: “Kama huwezi kuwashinda jiunge nao”.

Kwa mujibu wa Dk Chikwem hivi sasa mashirika makubwa ya Nigeria kama Shell, Mobil, Chevron, Texaco, Citibank, Accenture, Nestle, Cadbury, Guinness yanapendelea kuajiri wahitimu wa vyuo vya nje ya Nigeria. Mashirika haya hayana imani tena na mfumo wa elimu pamoja na wahitimu wa Ni-geria.
 
Ujumbe umefika mkuu, usione tupo kimya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…