Ngono ya mdomo chanzo kansa ya Koo

Ngono ya mdomo chanzo kansa ya Koo

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
70,791
Reaction score
98,334
"Kansa inayoongoza kwa Tanzania ni Kansa ya Shingo ya Kizazi. Kuna baadhi ya Kansa zinasababishwa na kirusi anayeitwa HPV. Kirusi huyu anaambukizwa kwa njia ya ngono kama vile mtu anavyopata HIV. Huyu HPV ameonekana kushirikishwa kwenye Kansa ya Shingo ya Kizazi ambayo inaoongoza hapa Tanzania.

"Pia kuna Kansa ya mfumo wa upumuaji ipo kwenye kimeo na yenyewe pia inahusishwa na huyo Kirusi. Kwahiyo tukiwa na ngono salama hatutajikinga na HIV peke yake. Na huyu kirusi wa HPV wanawake wengi wanapata kwa sababu wanaume wanabeba yule Kirusi na akiwa anafanya ngono na wanawake wengi anasambaza.

Kwa sasa hivi kuna chanjo zimeanzia kutolewa kwa mabinti wadogo chini ya Miaka 14 kwa ajili ya kupunguza uwezekano wa Saratani ya Kansa ya Kizazi. Ngono kwa njia ya mdomo ni chanzo cha Kansa ya Koo ya mfumo wa upumuaji" - Dr. Evelyne Mkuchika, Daktari bingwa wa saratani Taasisi ya saratani Ocean Road.

#LiveonClouds360
20230607_210100.jpg
 
"Kansa inayoongoza kwa Tanzania ni Kansa ya Shingo ya Kizazi. Kuna baadhi ya Kansa zinasababishwa na kirusi anayeitwa HPV. Kirusi huyu anaambukizwa kwa njia ya ngono kama vile mtu anavyopata HIV. Huyu HPV ameonekana kushirikishwa kwenye Kansa ya Shingo ya Kizazi ambayo inaoongoza hapa Tanzania.
Jamani sasa tusizame tena chumvini? Kha sasa dunia ina raha gani tena
 
Back
Top Bottom