Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Ngorongoro Heroes ambayo ipo kundi C pamoja na Ghana , Morocco na Gambia, inashika nafasi ya mwisho baada ya kupoteza dhidi ya Ghana goli 4-0 . Nafasi ya tatu inashikwa na Gambia ambaye naye alipoteza dhidi ya Morocco goli 1-0.
Ghana ndiye kinara katika kundi hilo ambaye naye atashuka dimbani hapo kesho kupepetana na Morocco.
Michezo mingine itachezwa hii leo ya kundi B , hili ni kundi ambalo michezo yake miwili ya ufunguzi ilimalizika kwa sare.
Kwahiyo timu zote zina alama 1, Namibia anashika nafasi ya juu akifuatiwa na Jamhuri ya Afrika ya kati hii ni baada ya kutoka sare ya 1-1 na Tunisia anashika nafasi ya 3 akifatiwa na Burkina Faso hii ni baada ya kutoka sare ya bila kufungana.
Katika michezo ya leo Tunisia atakutana na Namibia huku Jamhuri ya Afrika ya kati atakuwa nyumbani kukipiga na Burkina Faso.