Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Timu ya Taifa ya Tanzania vijana umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes imeendelea kusuasua kwenye mashindano ya Afcon u-20 baada ya kucheza michezo miwili na kuambulia alama 1.
Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Ghana juma lililopita, hii leo imetoka sare ya 1-1 na Gambia.
Kwa matokeo hayo Ngorongoro heroes inashika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi C.
Ghana ambaye anaongoza kundi hilo ana alama 4 kama Morocco huku Gambia akiwa na alama 1 kama Tanzania .
Ngorongoro Heroes ndio timu pekee kwenye kundi hilo iliyoruhusu magoli mengi zaidi ambayo ni 5 ikifuatiwa na Gambia iliyoruhusu 2 huku Morocco na Ghana zikiwa hazijaruhusu kabisa goli.