Ngorongoro (NCAA) offisi ya Arusha iongezewe majukumu

Ngorongoro (NCAA) offisi ya Arusha iongezewe majukumu

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Wapendwa
kwa mdau yeyote anaye laza wageni ndani ya ngorongoro na kutakiwa kulipa camping fees atakubaliana na mimi kuwa ni kero isiyovumilika

1. Wageni hawaruhusiwi kuingia ndani ya hifadhi kama watalala ndani ya camps bila kulipia hiyo gharama (camping fees $50)- ambapo ni sawa tatizo hapo ni kuwa hayo malipo yanafanyika benk ila Voucher (GRR) inatoka Makao makuu ambapo ni Ngorongoro.

Fikiria umepata wageni wawili na wanataka kwenda park? Sijui kama wanafikiria gharama ya kutoa gari Arusha hadi Ngorongoro umbali wa km karibia 200 na kurudi? ili kupata tu camping fees Voucher???
Kwa nini hivyo vibali camping fees visitoke Arusha??


2. Kero nyingine hii ni ya geti la Loduare
Pale unapokuta magari kama 60 getini muda wa 06h00 halafu yupo karani mmoja. wakati ndio muda rasmi wa kufungua gate...

Wageni wanaishia kusubiri kwa masaa kadhaa? tuna pata aibu jamani...hili nalo ni hadi Magufuli awasaidie?

 
Nadhani wahusika, watalifanyia kazi hili
 
Back
Top Bottom