Ngorongoro ni mali ya Maasai wa Tanzania na Kenya

Ngorongoro ni mali ya Maasai wa Tanzania na Kenya

broken ages

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2012
Posts
235
Reaction score
84
WATANZANIA hatuko tayari kupaza sauti kuwatetea wachache mnaopigania kuiharibu NGORONGORO kwa faida na ubinafsi wenu bila kuyatizama maslahi mapana ya TANZANIA leo na kesho

Na badala yake tutawashaurini kuondoka ili maisha yaendelee kwanini mnatetea kuishi porini ambapo kuwepo kwenu kutasababisha wanyama waondoke? Ama ninyi siyo WATANZANIA wenzetu? Ninyi ni mamluki ama wahamiaji haramu kutoka nchi nyingine?

Na kama ni WATANZANIA mbona hamjali wala kuona faida ya kuwa na NGORONGORO yenye kustawi na kuzalisha kipato kwa ajili ya WATANZANIA wote?

Ktk kuishi kwenu ngorongoro ninyi wachache na mifugo yenu michache ukilinganisha na fedha za kigeni zipatikanazo ngorongoro kutokana na vivutio vya utalii ikiwa ni pamoja na mazingira na wanyama ni kipi chenye faida kubwa zaidi kwa WATANZANIA milioni 60?.

Mnakohamishiwa ni ndani ya mipaka ya TANZANIA na siyo nje mnahamishiwa kwenye maeneo ambako ndiko tunakoishi sisi WATANZANIA wenzenu na mmewekewa miundo mbinu mizuri ambayo ni mahitaji muhimu kwa maisha ya binadamu maji, umeme, hospitali shule na mambo mengine muhimu. Je, mnataka tupaze sauti tuseme nini kwa serikali?

Je, mnashauri nini ninyi kwamba wahame wanyama na bonde la ngorongoro nalo lihame? Kati yenu na wanyama ni nani alimfuata mwingine NGORONGORO?

Ukizingatia kwamba huwezi tofautisha Masai kutoka KENYA na TANZANIA kunao uwezekano mkubwa kwamba wamasai wa TANZANIA wamechochewa na kuhamasishwa na wenzao kutoka KENYA kufanya migomo na vurugu kwa nia ya kuchelewesha ama kuzuia zoezi la kuweka alama za mipaka NGORONGORO ambalo lilikuwa ni kwa nia ya kuendeleza na kuistawisha NGORONGORO

Kutokana pengine na faida ambazo Masai wa jirani walikuwa wanazipata kwa NGORONGORO kwa kulisha mifugo yao ama pengine kunao watu wako nyuma ya hao Masai wa Kenya kwa sababu za ushindani wa kibiashara wanatumika kuwachochea wenzao wa TANZANIA ili kuendeleza uharibifu wa mazingira ya NGORONGORO.

Tunawasihi ndugu zetu Masai wa TANZANIA kushikamana mkono na Serikali na kutoa ushirikiano ili tuitunze na tuilinde NGORONGORO kwa faida ya kizazi hiki na hata kizazi kijacho cha TANZANIA na wala wasikubali kutumika na wageni kutoka nje

Pia tunawasihi wale ambao wamekimbilia ama wamerudi kwao Kenya kwa kisingizio cha kwenda kutibiwa basi wabakie huko na wala wasije tena huku kuja kutuletea vurugu nayo Serikali iwe macho mipakani ili wasije tena kwetu kisababisha vurugu.
 
Wamasai kuwa ngorongoro wamesaidia ulinzi wa mali asili zetu. Wakiondoka hakuna atakayeona uporaji wa wanyama hai hivyo kupiga kelele!! Linatafutwa giza!!
 
WATANZANIA hatuko tayari kupaza sauti kuwatetea wachache mnaopigania kuiharibu NGORONGORO kwa faida na ubinafsi wenu bila kuyatizama maslahi mapana ya TANZANIA leo na kesho
Ukitaka kujua kuwa wanatumika angalia hiyo barua halafu wanakuja kutupigia pigia kelele tu humu
 

Attachments

  • IMG-20220614-WA0034.jpg
    IMG-20220614-WA0034.jpg
    73.2 KB · Views: 26
Hakuna mmsai hata mmoja anaeishi huko ngoro ngoro mwenye smart phone na kama yupo basi hana jamii forum app,na ikitokea ana jamii forum App basi hajui kiswahili. So ujumbe wako hautawafikia .

Hilo eneo ni hako ya wamasai, kuhusu fedha za kigeni vivutio vipo vingi Tz kwann wasionyeshe mfano wa kksanya hayo mapato kwa wingi huko?

Hivi Tz yenye wangu 60 milion ni waku shindwa idadi ya watalii na fedha za kigeni na nchi ndogo kama shelisheli yenye watu wasio zidi hata 10 milion?ilhali wao wanategmea tu fukwe na mahoteli?

Sisi tuna fukwe ngapi nchini hapa mbona zote hovyo?Sisi ni miongoni mwa nchi 3 Africa zenye vivutio vingi zaidi lkn mapato na idadi ya watalii inatia kinyaa. Ndo mmeona solution ya hilo ni kuwaondoa wamasai kwa wamasai kwa kuwatesa?

The problem sio wamasai, bali ni ukosefu wa elimu ya maono "Visionary Education "kwa viongozi wetu na umbumbumbu wa watanzania.Edoward Lowasa alisema matatzoulimu matatu makubwa tulio nayo ni 1.Elimu 2. Elimu 3.Elimu.
 
Huyu kama sio Piraaaa wa altareni, sijuiiii
 
Halafu wamasai wanajiona wao wanayo haki ya kuishi maporini kulilo haki ya wanyama kuishi huko.
lazima tupaze sauti kuilinda ngorongoro na hayo ndio maslahi mapana ya nchi yetu.hatuwezi kulinda maslahi ya mamluki wachache kwa faida yao.tunajua kwa undani kinachoendelea huko ngorongoro.ni unafiki na ni ujinga kutetea wapuuzi wachache kwa ajili ya matumbo yao.hao wanaoshirikiana kuchochea vurugu ngorongoro ni wapuuzi wachache wa ndani na nje ya nchi ambao wamewekeza vimifugo koko pale ngorongoro kwa ubinafsi wao,mifugo ambayo haichangii chochote ktk uchumi wa nchi hii.serikali iwapuuze hao watu na iangalie maslahi ya walio wengi kinyume na hilo tutaendelea kufuga donda ndugu huko mbeleni.Aluta Continua kazi na iendelee.
 
Wakenya wengi wanaojifanya watanzania hapa JF, tumeshaanza kuwaelewa kupitia hili seke seke la Ngorongoro. Kuna huyu anaejiita waziri mkuu butu wa Israel (sina haja ya kuandika jina lake) maana anafahamika na asha comment matapishi ili kuwatetea ndugu zake waendelee kuwepo katika ardhi yetu kwa kisingizio cha umasai na utanzania wa mchongo. Btw.. Hakuna mmasai mwenye asili ya Tanzania ambae anaweza kuacha kwenda kuishi katika maeneo mazuri yenye mazingira mazuri, na miundo mbinu mizuri kama nyumba nzuri, hospital nzuri, barabara, maji, umeme nk, afu eti akimbilie Kenya kwenda kuishi ukimbizini. Hii haingii akilini na ukizingatia maisha ya ukimbizi kila mtu anayajua (nenda au google kuhusu maisha ya wasomali huko katika kambi za kenya). Kifupi hakuna mtu ambae anaweza kuwa tayari kwenda kuishi maisha ya ukimbizi nje ya nchi huku akiacha ofa ya kupewa nyumba ya bure na serikali yake. So hao walioenda Kenya bila shaka au chenga ni wakenya waliokuwa wakiishi Tanzania kwa kimvuli cha ujirani mwema na uraia wa mchongo. Serikali isirudi nyuma kamwe, na ikithubutu kusitisha oparation hii yenye faida kwa taifa, sisi wenye uchungu na nchi hii, na tunaopinga nchi yetu kuendelea kufanywa shamba la bibi na wamasai wa mchongo tutaandamana. Nimeweka picha za nyumba walizojengewa na serikali ambazo wamasai wa mchongo wanadai hawazitaki, na chini nimeweka picha ya maisha ya kambi ya wakimbizi huko Kenya, ambapo eti wamasai wa mchongo wamekimbilia huko wakaishi maisha ya ukimbizi kama wanavyoishi wakimbizi wenzao original. Poleni wakenya, hii ni karne ya 21 hakuna tena ujanja ujanja na uigizaji wa kijinga kama huu mnaofanya, utakaoweza kutufanya wenye akili timamu tuingie chaka kizembe.
 

Attachments

  • images (14).jpeg
    images (14).jpeg
    37.2 KB · Views: 19
  • images (34).jpeg
    images (34).jpeg
    33.1 KB · Views: 12
  • images (67).jpeg
    images (67).jpeg
    11.8 KB · Views: 12
  • images (76).jpeg
    images (76).jpeg
    36.2 KB · Views: 17
Wewe unajua wakitaka kuoa, moran inabidi afanyeje??
Na wanamaliza malisho ya wanyama pori kwa ng'ombe wao wanaozurura hovyo. Nomadic pastoralism karne ya 21 ni ujinga. Huko Pwani na Morogoro kila siku kulishia mifugo ktk mashamba ya wakulima na kuwapiga juu. Waharibifu sana wa mazingira, waondolewe mbona sisi tiliondolewa vijiji vya asili tukapelekwa vijiji vya ujamaa. Pesa za utalii zitainua uchumi elimu na afya/matibabu.
 
Wamasai kuwa ngorongoro wamesaidia ulinzi wa mali asili zetu. Wakiondoka hakuna atakayeona uporaji wa wanyama hai hivyo kupiga kelele!! Linatafutwa giza!!
No no no. Ulinzi haikuwa primary objective, ilikuwa ni kuishi tu. But today mamlaka ina askari wake.
 
Back
Top Bottom