Ngorongoro uchochezi unatokea wapi?

Ngorongoro uchochezi unatokea wapi?

broken ages

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2012
Posts
235
Reaction score
84
kinachoendelea Ngorongoro ni vita vya kiuchumi hivyo Watanzania tunapaswa kufungua macho kwa sababu siamini kama serikali itaonea ama itapenda kuumiza raia wake bila sababu ya msingi.

Kwa maana kuna taarifa kwamba serikali iliandaa eneo huko Handeni kwa ajili ya kuwahamishia huko Wamasai kutoka Loliondo na tena serkali ikaweka mazingira mazuri ya kuishi kwa kuwajengea nyumba bure wananchi hao ili waweze kwenda kuishi bila shida na hili limefanyika kwa nia njema kabisa.

Kwamba wananchi wapate maisha ambayo ni salama lakini pia ili waweze kupisha wanyama wanaotusaidia katika pato la taifa kwa maana ya kwamba kututangaza ktk nyanja ya utalii nalo liweze kuendelea na kustawi kwa maana ya kwamba NGORONGORO izidi kudumu.

Cha kushangaza ni upinzani uaojitokeza na unaoonekana kutoka kwa wakazi pamoja na uungwaji mkono unaotoka kwa raia ama wale wanaojiita ni watetezi wa haki za binadamu jambo ambalo linafanya zoezi la kuhamisha kuwa ni gumu kidogo

Na hao wanaofanya hivyo wanapinga tu bila kutoa ushauri wa nini kifanyike zaidi ni kwamba wamebakia tu kusisitiza kwamba raia wasihamishwe

Mimi naona badala ya kushinda tukisema na serikali kwamba isihamishe raia ni bora tungewashauri masai kuhama kwa hiyari na hasa ukizingatia kwamba ktk makazi hayo mapya wameboreshewa huduma na nyumba waejengewa pia ni ndani ya ardhi ya Tanzania kwa maana haiwezekani waendelee kuharibu ama kuua hifadhi wakati bado kunazo sehemu za kuishi nje na hiyo hifadhi

Watanzania tuungane na serikali kuhamasisha wamasai kuhama loliondo maana hawana wanachopoteza iwapo watahama.

Tusikubali kupokea propaganda za kutoka nje kwa majirani ambao kwa sababu ya vita vya kiuchumi wanafanya kila mbinu kuuzima mpango wa serikali ya Tanzania.

Naamini serikali kwa nia njema imepima kwa mapana kabisa kwamba ni lipi lifanyike kwa faida pana na ya muda mrefu kwa taifa kwani kama ingewezekana basi.

Wangejamishwa wanyama ili wabaki binadamu ambalo haliwezekani kwani kunao uwezekano mkubwa sana wa binadamu kuhama na bado maisha yakaendelea kwa ubora zaidi.

 
Serikali ya Tanzagiza inajua kuficha mateso na matatizo yao ndani ya kauli “ Hii ni vita ya kiuchumi”
 
Back
Top Bottom