Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 966
- 6,019
Wasaalam Wadau wa Jukwaa letu hili 🤝
WAZIRI DKT. GWAJIMA AZINDUA BARAZA JIPYA NGOs
Source; Na WMJJWM, Dodoma, @maendeleoyajami @nacongotz
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito kwa Viongozi na Wajumbe wote wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo.
Ametoa wito huo wakati akizindua Baraza jipya la Mashirika hayo Juni 25, 2024 jijini Dodoma baada ya kumalizika kwa muda wa Baraza lililozinduliwa mwaka 2021 chini ya aliyekuwa mwenyekiti Dkt. Lilian Badi ambaye amepokelewa ‘kijiti’ na Ndg. Jasper Makala.
Waziri. Dkt. Gwajima amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo ili kukidhi matarajio ya jamii ya Watanzania kwa ujumla.
"Itakumbukwa kwamba, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yamekuwa yakitekeleza miradi na afua katika maeneo mbalimbali ya kiutekelezaji, ikiwa ni pamoja na sekta ya afya, kilimo, elimu, maji, mazingira, utawala bora, nishati, uhifadhi wa jamii, uwezeshaji wa jamii na sekta nyingine mtambuka." Amesema Waziri Dkt. Gwajima.
Amesema, suala la mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wapya wa baraza, yapo ndani ya uwezo wa Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali limeanzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 25(1) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Sura ya 56 ya Sheria za Tanzania. Kwa mujibu wa Kanuni 5(a)(iv), 5(b)(ii) na 5(c)(v) ya Kanuni za Uchaguzi za Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali za mwaka 2016, Baraza linatakiwa kufanya Uchaguzi kila baada ya miaka mitatu (03).
MWISHO