Source; Na WMJJWM, Dodoma, @maendeleoyajami @nacongotz
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito kwa Viongozi na Wajumbe wote wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uzalendo.
Ametoa wito huo wakati akizindua Baraza jipya la Mashirika hayo Juni 25, 2024 jijini Dodoma baada ya kumalizika kwa muda wa Baraza lililozinduliwa mwaka 2021 chini ya aliyekuwa mwenyekiti Dkt. Lilian Badi ambaye amepokelewa βkijitiβ na Ndg. Jasper Makala.
Waziri. Dkt. Gwajima amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo ili kukidhi matarajio ya jamii ya Watanzania kwa ujumla.
"Itakumbukwa kwamba, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yamekuwa yakitekeleza miradi na afua katika maeneo mbalimbali ya kiutekelezaji, ikiwa ni pamoja na sekta ya afya, kilimo, elimu, maji, mazingira, utawala bora, nishati, uhifadhi wa jamii, uwezeshaji wa jamii na sekta nyingine mtambuka." Amesema Waziri Dkt. Gwajima.
Amesema, suala la mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wapya wa baraza, yapo ndani ya uwezo wa Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali limeanzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 25(1) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Sura ya 56 ya Sheria za Tanzania. Kwa mujibu wa Kanuni 5(a)(iv), 5(b)(ii) na 5(c)(v) ya Kanuni za Uchaguzi za Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali za mwaka 2016, Baraza linatakiwa kufanya Uchaguzi kila baada ya miaka mitatu (03).
π Swali zuri. Soma sheria husika Iko miaka mingi huu ni utaratibu tu wa kawaida. Nimealikwa kuzindua. Sasa ndugu yangu ulitaka niseme siji au? Mwenzako sijaelewa tafadhali...
Suala la hiyo foundation ni la kisheria chini ya sheria ya usajili wa NGO. Wakimaliza utaratibu watatoa taarifa utaona tu. Mambo yote ni kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Kanuni siyo kwa mujibu wangu mimi kama mimi hapa. Ahsante kwa utashi wa kutaka kufuatilia taarifa za wizara yako ya jamii. π€
π Swali zuri. Soma sheria husika Iko miaka mingi huu ni utaratibu tu wa kawaida. Nimealikwa kuzindua. Sasa ndugu yangu ulitaka niseme siji au? Mwenzako sijaelewa tafadhali...
Mimi naomba nikuulize swali kuhusu hawa vijana wanaojiuza maarufu kama Vyangudoa, dada poa au kaka poa, sijui ipi ni formal na ipi ni informal lakini nadhani tuko pamoja.
Mimi siyo mwanasheria ila jamii haipendezwi na biashara yao. Wewe Dr.Gwajima kama waziri, kutokana na usugu wa hawa vijana kukataa kuacha.
Wizara unayoiongoza hamuoni kama kuna haja ya kuanzisha au kutunga sheria kuruhusu biashara hiyo kwa kusajiri madangulo/brothel houses ambazo watoa huduma na wafuata huduma wakutane huko kwa faragha zao?
Kuna baadhi ya nchi kwa kupinga kujiuza hadharani waliruhusu maeneo kama hayo(brothel houses), ili wapendao waende huko, na wasiwe barabarani usiku, badala yake waende huko kutakako kuwa kumeruhusiwa.
Watoa huduma wapimwe kuhakikisha wako salama, hapa namaanisha magonjwa ya zinaa na mengine yanayoambukiza.
Sijui wewe binafsi unazungumziaje, au wewe kama waziri, hilo unalionaje?.