Ngozoma Matunda afariki dunia

Ngozoma Matunda afariki dunia

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Imetolewa mara ya mwisho: 19.11.2008 0116 EAT

• Ngozoma Matunda afariki dunia

Na Elizabeth Mayemba
Majira

MAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Rashid Ngozoma Matunda (75)amefariki dunia.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Mengi Matunda ambaye ni kipa wa zamani ya Yanga, alisema baba yake alikutwa na mauti jana mchana kwenye hospitali ya Mwananyamala, ambapo alianza kuumwa malaria juzi.

Alisema kutokana na ugonjwa huo jana asubuhi hali yake ilibadilika, hivyo wakampeleka Mwananyamala Hospitali, ambapo walielezwa alikuwa na shinikizo la damu na mauti kumkuta saa chache baadaye.

Alisema mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo mchana kwenda Morogoro kwa ajili ya mazishi na kuongeza kuwa ameacha wajane wawili, watoto 17 na wajukuu kadhaa ambao idadi yake hakuweza kukumbuka mara moja.

Akizungumzia msiba huo, Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Iman Madega, alisema ni pigo kwao, kwa kuwa marehemu ameacha pengo kubwa kwa klabu hiyo.

"Tumeshtushwa sana na msiba huu, kwani hatukuwa na taarifa za kuumwa kwake, lakini familia ilituambia hakuugua muda mrefu,"alisema Madega.

Matunda atakumbukwa kwa uongozi wake shupavu miaka ya nyuma akiwa Mwenyekiti kwa nyakati tofauti na kujijengea jina kwa timu yake kujipatia ushindi kila ilipokutana na Simba, ambapo hata alipochaguliwa kwa wadhifa wa Makamu Mwenyekiti Mei mwaka jana suala la kuifunga Simba ilikuwa moja ya sera zake.
 
Mungu amlaze mahala pema peponi... Wanayanga tutakukumbuka daima...
 
Ulazwe mahali pema peponi Ngozoma.
 
RIP Mzee Rashid Ngozoma Matunda,Wapenda michezo wote tutakukumbuka Daima!!!
 
Msiba mkubwa kwetu washabiki wa jangwani M/mungu amlaze mahala pema peponi Ameen
 
Mja atalipwa akhera kwa amali zake duniani, M/Mungu amrehemu mja wake. AAMINA
 
Back
Top Bottom