Nguo na Mitindo ya Zamani ambayo kwa sasa ukivaa ni kituko

suruali za "don't touch my shoe" kwa akina kaka

ila fashion nyingi zinarudi, leo hii jaribu kuvaa suruali ya bugaloo mtaani uone kesho yake tu watu kibao watakuwa wameiga. hata raizon na viatu vya wanchoma kumoyo vyote sasa hivi ni fashion
 
Chupi za VIP zimekumbusha mbali sana!! mafuta ya shanti, yolanda unajipaka siku maalum ukiwa na kidate, we acha tu, maisha haya, Mungu anajua!
 
Kulikuwa na suruali za jeans za kubana 'Dangrese"
kama zile za Bob
 
Hizi ulikuwa ukifua zinapaa(kuwa ndogo) bana, yangu nikaongezea na kitambaa cha rangi tofauti kwa chini.. hahahaaaa bonge la mtoko na viatu vya TAFU (e.g Benqi).

Unazungumzia NDOPA enzi tunavaa suruali za TOKYO, BIG SAM; Usipokuwanayo sikukuu hata pilau halipandi.
 
Mimi nilikuwa nadhani kuwa humu jukwaani naongoza kwa utu uzima, kumbe hapana, kumbe nami pia nina kaka zangu humu. Viatu vile vya Raise On, miaka ya mwanzoni mwa themanini pamoja na saa zile za disco. Baadaye sasa ndiyo zikaja suruali Michael Jackson, zikafuatiwa na zile zenye celebration unavalia tumboni. Jeans aina ya Lee nimeivaa mwaka 1983 pamoja na viatu vyaraba mtoni, soli ikiwa ina meno kama ya mamba, halafu ni ya kandambili hizi za kawaida.
 
Shati la ndege, moro shoes, tinabuu, dontach (don't touch), asante mchaga kiatu, safari boot na viatu vya mataili ya gari
Mkuu Zatara dontach saizi imerudi kwa kasi sana vijana wajanja wa town wanatupia hizo ni 🔥🔥
 
hyo crimplin alikua anaisema mama yangu sijui ata ni vazi gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…