Ngurumo: Magufuli na “maparoko wake” wana kesi ya kujibu

Kumbe hauna uhakika?!

Kwaiyo katiba inasema raisi akiingia nyumba ya ibada anakuwa sio raisi?
Anakuwa muumini Wa kawaida tu chini ya padre ama mchumgaji lusekelo.

U Rais ankuwa nao ila hana mamlaka akiwa ndani ya hizo nyumba za ibada,labda kanisa ndo limwalike madhabahuni asalime waumini sio ahutubie wananchi madhabauni maana dini na siasa havichangamani.
 
Nyie ndio mtaji Wa hicho chama chakavu,yaani ni kusifu na kuabudu tu hata kwa mambo yanayokosewa.
Kina dada bhana, yaani nyie ndiyo Maana vijana huwa hawahangaiki kujua huyu kamaYuko tayari Kwa kile anataka kabla hata hajamtongoza, sasa wewe! Unaongea mambo ya chama Nani kakuuliza?
 
Kama akina Bagonza, Ponda, Mwamakula wanatumiwa nyadhifa zao za kidini kuongea mambo ya kisiasa kwenye membari zao, kutakuwa na uhalali gani wa kuwazuia wanasiasa, hasa wenye nyadhifa kubwa, kuzungumzia mambo ya kidini kwenye majukwaa yoyote wanayoona yanafaa?
 
Kikubwa asiwe anapewa nafasi ya kuhutibia kanisani
 
Wengi wa kwenye huu uzi ni wanao lipwa kueneza udanganyifu kwa wananchi ili kuingia mtegoni.

Tumestuka,ugonjwa hata kama upo basi si wa kiwango kisemwacho na tunaweza tukauishi kama Malaria.

Barakoa tutavaa za vitenge au T-shirt yangu nitaichana nijifunge mwenyewe puani. Huku mitaani watu tumelundikana sokoni na vijiwe vya kahawa na hakuna mwenye mafua wala kikohozi labda cha kawaida kama siku zote.
 
Corona IPO jamii forum Tu. Huku mtaani hata habari hatuna
Ipo kweli...na kujikinga nayo ni wewe mwenyewe kuchukua tahadhari kwa mujibu wa maelekezo ya wataalamu wa afya, na si kusubili kuambiwa takwimu za walioambukizwa, waliokufa na waliowekwa karantini!
Kumbuka kauli za viongozi wa kisiasa na kidini ni za ziada tu kwako!
Usiache watu wengine wakushikie akili zako....Chukua hatua.
 
Chunga sana huo mdomo wako unaotoa maneno yanayotoa harufu mbaya.Eti uko kwenye mfungo.Mfungo gani huo,huo ni mfungo wa shetani kamili.Kajifunze kanuni za kufunga.Waulize wanaofunga wanabugia kila saa kama wewe.Poleeeeeeee
Anashinda njaa tu sio kufunga.
 
Tumeisikiliza hotuba vizuri, hakuna mahala ambapo anawaswaga na kuwapelekesha mapadre na maaskofu Katoliki. Rais ametoa tahadhali juu ya kutumia barakoa zinazostahili.

Mtoa mada huna lolote, endelea kuosha vgombo vya wazungu huko ughaibuni.
jaman mmeisikia hii pimbi,usikute mwenye hii ID ni magufuli mwenyew
 
Wenye macho hawaambiwi tazama, usishangae kuna mtu alimfuata Padre na kumwagiza kimyakimya
 
Kumuelewa mzee baba Ni ngumu

Anadai tumtegemee MUNGU tu dhidi ya korona lakini yeye anaingia kanisani walinzi wenye silaha za Moto

Anaogopa Nini? Si amtegemee MUNGU tu

Anadai anayetaka kuiponya nafsi yake anaingamiza .je yeye kuingia na mitutu na silaha za kivita kanisani anaingamiza au anilaiponya nafsi yake ?

Mi mwenzenu simuelewi kabisa [emoji1]

Tuendelee kupiga nyonga covid ipo[emoji1]
 
Nachukia sana hawa waosha vyombo wa wazungu kuja kutushauru. Endeleani kuosha vyombo hamna lolote.
 

Uko sahihi na nakubaliana na wewe. Lakini nina hoja moja au mbili...

Kwamba, kwenye makanisa yetu (sijui utaratibu wa misikini kwa sababu mimi sio mwislamu), uko utaratibu wa kukaribisha wageni wote bila kujali hadhi ya mgeni huyo na hupewa nafasi kusalimia...

Kosa wanalofanya baadhi ya vingozi wa makanisa ni kuruhusu viongozi ambao hawajapakwa mafuta ya kuhudumu kusimama madhabahuni na kuinajisi madhabahu...

Kiongozi Mkubwa kama Rais, Waziri Mkuu, Spika, Jaji Mkuu au waziri fulani anapotembelea kanisa lenu kuabudu pamoja nanyi ni jambo jema na siyo mbaya na siyo dhambi kumpa nafasi maalumu ya kusalimia waumini...

Na inatakiwa asalimie akiwa amesimama mahali hapo hapo alipokaa. Ni marufuku kabisa kupewa ama kuitumia mimbari (madhabahu) kufanya kama anavyofanya Rais Magufuli kukosoa au kuingilia taratibu za kanisa, kushambulia ama kukejeli viongozi wa kanisa la Bwana...

Anatakiwa kuwa na busara na hekima. Asijiinue ama kujikweza. Atambue kuwa mamlaka na madaraka yake ya Urais in kwa ajili ufalme wa hapa duniani...

Kamwe, hayaingiliani kabisa na madaraka na mamlaka ya wateule wa ufalme wa mbinguni waliopo hapa duniani kwa sababu utendaji na taratibu za falme hizi mbili (wa mbinguni na wa duniani) ni tofauti kabisa....
 
Nachukia sana hawa waosha vyombo wa wazungu kuja kutushauru. Endeleani kuosha vyombo hamna lolote.
Ni kwa vile hujatembea. Ungelikuwa na exposure , basi ungejua kuwa kuosha vyombo ni kazi (ajira). Ambayo hapa jamaa ameshindwa kuitoa.
 
Kule kenya mlikozowea kutolea mifano ya siasa bora ya DEMOKRASIA.

WAO SIO TU WANATUMIA MIMBARI KUHUTUBIA SIASA
,BALI HADI MAKONDE WANATWANGANA MISIBANI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…