SoC01 Ngurumo ndani ya msitu mnene

SoC01 Ngurumo ndani ya msitu mnene

Stories of Change - 2021 Competition

Fatina Suleiman

New Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
2
Reaction score
0
NGURUMO NDANI YA MSITU MNENE

“Mgeni aje mwenyeji apone”,,, usemi huu maarufu uliotumiwa na kuturithisha kwa miaka mingi hakika tumekua na tumeishi nao. Mgeni alietujia ni mgeni aliyejaa vitendawili visivyotegulika, ni mgeni asiejulikana wapi katoka na wapi anaelekea na kubadilisha maana nzima ya usemi usemao mgeni aje mwenyeji apone na kuwa mgeni aje na mwenyeji asahaulike, hakika ni ngurumo mwituni, ngurumo hii haijulikani itokapo wala iishiapo. Huyu mgeni si mwingine Ni virusi vya uviko 19 [COVID 19] mgeni Alie kuja mwishoni mwa mwaka 2019.

Virusi vya korona ni jamii kubwa ya virusi vilivyojulikana kusababisha magonjwa yanayo anzia na homa ya kawaida hadi homa kali, kama vile homa kali ya upumuaji ya mashariki ya kati [MERS] na homa kali ya mfumo wa upumuaji [SARS].

Viligunduliwa 2019 huko Wuhan, China. Hivi ni virusi vipya vya uviko ambavyo havijatambuliwa hapo awali kwa wanadamu.

Virusi hivi vinasambaa kwa Ugonjwa uliopewa kipaumbele kisicho cha kawaida, umesimamisha mataifa yote . Mataifa yalioendelea na ambayo ndo yanakuwa kiuchumi, Mgeni huyu amefanya wenyeji kusahaulika na kusababisha sintofahamu kwani waliohasirika na magonjwa wenyeji wameshindwa kujua nijikomboe kwa vipi kwani kila atakapo kwenda ni Mgeni ndo anatakiwa. Kwa kuwa kila mmoja anajitetea kwalake pengine silaha yako ndo ingekuponya kwa wakati huu.

Mgeni huyu amekuja kwa muda mfupi lakini ametawala kwa muda mfupi na kupatikana kwa chanjo lakini mwenyeji bado anaishi kwa muda sasa ni hatari lakini bado hajapatiwa chanjo. Mwenyeji wetu ni [VVU]

Miongo kadhaa imepita tangu kuzuka kwa janga la Virusi vya Ukimwi, watafiti bado hawajafanikiwa kubuni formula ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo. Lakini sasa tunazo chanjo nane za uviko 19 katika muda wa miezi 18 tu. Tunabaki na maswali je tunaweza kuarakisha chanjo ya VVU, kama ilivyokua kwa virusi vya korona.

Mwenyeji huyu [UKIMWI] Ulitambuliwa mara ya kwanza na vituo vya kuzuia na kudhibiti Magonjwa huko Marekani mwaka 1981, ilihali kisababishi chake – VVU –kilitambuliwa mwanzoni mwa muongo huo nchini huko.

Kwanza kabisa tufahamu kuwa virusi hivi kwa nchini Marekani viligunduliwa na kupewa jina la HIV mwaka 1983, hapo unaweza kuona ni muda gani ulikua umepita baada ya vita ya pili vya dunia. Wakati huo inasemekana kuwa Afrika watu walikua tayari wameanza kupata ugonjwa huo tokea mwaka 1900.

UKIMWI hadi hivi sasa hauna chanjo wala tiba, lakini tunaweza kuuwepuka ugonjwa huu kwa kuachana na ngono ambayo huweza kusababisha ugonjwa huo, pia kujikinga kwa kuepuka kuchangia vifaa au vitu vyenye ncha kali.

Kutokuchukuliwa kwa kipaumbele cha ugonjwa huu utasababisha wale wanaoishi na ugonjwa huo nao kusahaulika na kusababisha madhara makubwa ivyo basi swali linabaki kwetu, nani alaumiwe…

Kikubwa kila ugonywa unamadhara yake kwahiyo yote yachukuliwe kwa uzito ili kuepukana na madhara makubwa yanayoweza kutuangamiza kwani uviko 19 ndio gonjwa lilio tiliwa mkazo kuliko gonjwa la UKIMWI.

Turudi nyuma tukae nakutazama wapi tumekwama ili tuweze kupambana na mwenyeji wetu pamoja na na mgeni wetu, kwa usambamba ili tushinde maadui watakao tuvamia.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom