Nguva jike hajatimiza ndoto yake ya kuonana na rais

Nguva jike hajatimiza ndoto yake ya kuonana na rais

Nguva Jike

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2018
Posts
1,226
Reaction score
1,757
Habari za jioni.

Basi tarehe 25.02.25 nguva jike akapashwa habari za ujio wa mama Samia Suluhu wilaya ya Kilindi Tanga.

Weeee! Nguva jike huyo mbio mbio kwenda Mabalanga Kilindi sehemu atakayofikia mama Samia Suluhu.Kawasha punda lake la kichina(pikipiki brakeless)

Mara ghafla kwenye kona kichakani dimbwi la maji hili hapa mguu kwenye brake pedal.Holaah! Kwenye maji tiii.Punda linaogelea dimbwini.

Haaa! Hapa leo sitoboi.Nyomi ya watu hapo Mabalanga.Komandoo wa kutosha kila kona.Hakuna hata kiti kimoja cha kukaa.Lengo ilikuwa nguva jike awe mbele kabisa Frontline ili amuone mama kirahisi.

Mmmh haya! Huyo nguva jike akaona isiwe shida akaenda kwenye screen kubwa kama solar panels akawa anamuangalia mama huku akisikitika kukosa kumuona mama alikuwa na maneno muhimu ya kuongea nae walau 5 minutes.

Nguva jike akaondoka akiwa na huzuni ya tangu 1992 pale uwanja wa TTC Korogwe Teachers College alipokosa kumuona Marehemu Ali Hasan Mwinyi.

Daaah! Lakini nguva jike hajakata tamaa atajaribu tena.[emoji24]
 
Back
Top Bottom