My beginning
Member
- May 31, 2023
- 11
- 8
Maliasili ni vitu ambavyo vipo asilia. Vitu hivi ni vitu vinavyotuzunguka lakini havijatengenezwa na mtu au taifa fulani. Asilimia kubwa tunategemea maliasili kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa nchi na taifa kwa ujumla.
Tanzania ni moja ya nchi iliyobarikiwa kuwa na maliasili nyingi kama vile misitu, ardhi ya wanyamapori na mbuga za wanyama, madini kama vile dhahabu,almasi, chuma, makaa ya mawe, nikeli, urani, gesi na tanzanite ambayo hupatikana Tanzania pekee duniani kote.
Tanzania kuna mito mingi kama vile mto pangani,mto mkomazi, mto weruweru, mto usa, mto ngarenaro, mto wami, mto Ruvu na mingine mingi. Tanzania ina mbuga nyingi za taifa kama vile hifadhi ya taifa arusha,hifadhi ya Gombe, hifadhi ya Katavi, hifadhi ya mikumi, hifadhi ya Ruaha, hifadhi ya mlima Kilimanjaro na nyingine nyingi ambapo zinashika karibu theluthi moja ya eneo lote la nchi.
Uchimbaji wa madini hufanya zaidi ya asilimia 50 ya jumla ya mauzo ya nje ya nchi ambayo sehemu kubwa inatokana na madini ambayo uchimbaji wake unazalisha mapato zaidi ya dola bilioni.
Tanzania ni nchi ya nne kwa kuzalisha dhahabu barani Afrika baada ya Afrika Kusini, Mali na Ghana. Mwaka 2010, asilimia 2 za uzalishaji wa dhahabu duniani zilitoka Tanzania na ikumbukwe kwamba Tanzania ndio nchi pekee duniani inayozalisha madini ya thamani ya Tanzanite.
Shida sio kwamba Tanzania imejaliwa maliasili nyingi namna gani ila ni kushindwa kujua kwa ufasaha nguvu iliyopo nyuma juu ya maliasili izo katika maendeleo ya nchi na kupelekea hasara au athari mbalimbali kwa maendeleo ya nchi.
Athari za kushindwa kujua nguvu iliyopo nyuma juu ya maliasili katika maendeleo ya nchi;
1. Kushuka kwa pato la Taifa.
Kutokana na kushindwa kujua nguvu kubwa iliyopo nyuma juu ya maliasili inapelekea kushuka kwa pato la taifa (GDP). Hii husababishwa na sababu mbalimbali ikiwepo utozaji kodi wa chini au juu zaidi na kupelekea uwekezaji mdogo wa watalii katika maaliasili kama vile mbuga za wanyama na madini. Hali ambayo inapelekea Tanzania kuwa na madeni mengi. Mwaka 2015, benki ya dunia iliipatia Tanzania mkopo wa dola millions 45 ili kuboresha sekta ya uchimbaji mdogo wa madini.
2. Makadirio ya bajeti serikalini kuwa makubwa.
Hii inatokana na ukweli kwamba Tanzania pamoja na kujaliwa maliasili nyingi bado inakuwa hakuna uthubutu wa kutumia nguvu au kuwekeza nguvu yote katika maliasili zilizopo.Hii hupelekea bajeti kubwa ya serikali kila ipangapo bajeti ya serikali kila mwaka. Mfano tunatakiwa kutumia miti shamba kwa ajili ya kutengeneza dawa mbalimbali hii itasaidia kupunguza bajeti kwenye upande wa sekta ya afya na kuacha kuagizia dawa nyingi kutoka nje ya nchi kwa sababu tayari kuna misitu mingi ambayo hutumika kutengeneza dawa mbalimbali.
3. Umasikini na madeni ya mara kwa mara.
Mara nyingi tunashuhudia serikali ya Tanzania ikipokea mikopo yenye thamani kubwa katika nchi mbalimbali na kubaki kuwa moja ya nchi tegemezi sana barani Afrika. Hii hutokana na kushindwa kujua nguvu kubwa ya maliasili zilizonazo katika maendeleo ya nchi. Mfano mwaka 2015, Benki ya dunia iliikopesha Tanzania dola million 45 ili kuboresha sekta ya uchimbaji mdogo wa madini lakini ukweli ni kwamba laiti serikali ingeendelea kupamabania nguvu juu ya maliasili ingeweza kusimama yenyewe. Takribani watanzania million 21.3 wanaishi chini ya mstari wa umaskini kwa sababu wengi wao hutegemea maliasili kuendesha maisha yao.
4. Unyonywaji wa nishati na madini.
Tangu ukoloni kulikuwa na unyonywaji wa maliasili mbalimbali kama vile madini katika nchi zisizo kuwa na maendelo. Hii tunalishuhudia mpaka sasa kumekuwa na unyonyaji wa maliasili Tanzania kama vile makaa ya mawe, mafuta na gesi asili pamoja na madini kama vile dhahabu, almasi, chuma, tanzanite na mengine mengi hali ambayo inapelekea kushuka kwa uchumi kwa sababu nchi tajiri za ubepari huchukua maliasili izo na kwenda kuuza kwa bei ghari kitu ambacho hupelekea mapato ya taifa yao kuwa ya juu.
Faida za kujua nguvu iliyopo nyuma juu ya maliasili katika maendeleo kwa taifa;
1. Ukuaji wa pato la Taifa.
Maliasili nyingi kama vile shughuli za uchimbaji madini na uchimbaji mawe zina mchango mkubwa sana katika ukuaji wa pato la taifa( GDP). Katika robo ya mwaka 2021 sekta ilirekodi asilimia 10.2 ya pato la taifa. Ukuaji huu husaidia maendeleo ya nchi katika sekta tofauti tofauti na itasaidia Tanzania kuepuka madeni ya mara kwa mara.
2. Kuendeleza uchumi wa nchi.
Utumiaji sahihi wa nguvu ya maliasili husaidia kuendeleza uchumi wa nchi na maendeleo kwa ujumla. Hii ni kwasababu ya ongezeko na mapato ya nchi kuwa makubwa hali ambayo upelekea uchumi kuwa mkubwa na uboreshaji wa sekta nyingine katika nchi kama vile miundombinu.
3. Ukingaji wa majanga na kuepusha migogoro.
Maliasili nyingi Tanzania zinaeza kutumika katika ukingaji wa majanga na kuepusha migogoro. Mfano misitu husaidia sana kukinga upepo hivo kuepusha atari za upepo mkali katika kilimo pia na uifanya ardhi ushikamane na hivyo kuzuia mmomonyoko wa udongo. Pia hisaidia kutatua migogoro mbalimbali kama vita ya unyonywaji wa malighafi na madini kwa nchi za kibepari.
4. Kupunguza gharama kubwa na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha serikalini.
Utumiaji sahihi wa maliasili kwa Tanzania husaidia kupunguza gharama kubwa na makadirio ya mapato na matumizi serikalini na husaidia kupanga bajeti yenye matumizi tija katika maendeleo mengine ya msingi katika nchi ambayo pia huchangiwa na asilimia kubwa ya pato kutokana na maliasili inayotuzunguka kama vile miti katika utengenezaji wa dawa, madini na maliasili nyingine.
5. Kuthibiti ongezeko la madeni kwa ujumla.
Utumiaji wa nguvu iliyopo nyuma juu ya maliasili itasaidia kuthibiti ongezeko kubwa lla madeni kwa Tanzania na kuifanya Tanzania isiwe moja ya nchi tegemezi kwa kutumia maliasili zilizobarikiwa. Hii itasaidia maendeleo katika sekta mbalimbali kama afya, elimu na miundombinu kwa ujumla kutokana na mstari wa kuvuka madeni.
Kwa hiyo, kwa Tanzania tuitakayo inatakiwa kutoza kodi kulingana na uwekezaji. Kodi hii husaidia pato la nchi na pia isiwe juu au chini ya uwekezaji kwani itafanya uwekezaji kuwa mdogo hali itakayopelekea kupungua kwa uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini. Mfano, raisi wa awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli aliweka sheria mpya katika sekta ya madini mwaka 2017 ikiwa ni pamoja na ushuru mkubwa kwa madini yanayosafirishwa nje ya nchi hali iliyopelekea kupungua kwa uwekezaji katika sekta ya madini. Pia itaitajika utungaji na utekelezaji wa sheria juu ya maliasili, hii itasaidia kutunza maliasili salama na kufanikisha maendeleo endelevu ya nchi. Vile vile ulinzi juu ya maliasili kama hifadhi za taifa hii itasaidia kupunguza ujangili kwa wanyama kama vile tembo na kifaru kati ya wanyama wanao saidia katika kukua kwa pato la taifa kupitia utalii.

Upvote
1