I'm Daniel
Hello JamiiAfrica.
Pole Kwa wale ambao wanapitia maisha na hali ngumu iwe Kwa makusudi au Mpango wa Mungu,
Mwenyezi Mungu awape wepesi,kila Jambo linalotokeq huwa na sababu zake naamini kila Jambo litapita
Ni siku nyingi zimepita sijakatiza Mitaa hii ,yaani jukwaa hili pendwa ,yaani app hii ambayo haina wafuasi wengi,ila ina magreat thinkers wengi Sana nimejifunza ,nimeburudika na kufurahia mengi kupitia jamiiforum.
Hizi ni zama za social networks,hizi ni zama za mitandao ya kijamii ,siyo zama za magazeti,radio na runinga ,siku hizi kama si PC,basi ni simu,iko wazi vyombo vingine vya habari vilipoteza mvuto zamani sana.
Mwanzo nilikuwa nabisha sana mtu akiikuta habari mitandaoni na kuniambia taifa zima lina habari,au limepata taarifa.
Nilidhani mitandao ina kundi dogo la watu ambao either ni wasomi or ni wajanja na watasha fulani.
Lahaulaaaah!
Sasa hivi kila mtu anapata taarifa tena ikiwa ni ya moto kabisa,yaani kila mtu yupo active na kinachoendelea kunako social networks.
Iwe ni habari ya udaku,umbea na serious issues zote watu wanapata Kwa wakati,hapa ni wengi wenye computer na wasiokuwa nazo,wenye simu na wasiokuwa nazo,kila mtu anapata taarifa Kwa wakati na kwa ukamilifu bila chenga.
My take
Tuwe makini na mitandao,
Mitandao inatunza kumbukumbu,
Mitandao inaaibisha,
Mitandao inafukua makaburi,
Mitandao inachonganisha
Mitandao haina Siri eti.
Mitandao inawakusanya watu PAMOJA .kumbukeni umoja ni nguvu
Ogopa sana watu wakiungana.
Sijui hata nimeandika nini,sijui ni pombe,,,aaaargh