Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,858
- 22,729
Nguvu ya Muziki
Kila moyo una wimbo. Pahali ambapo maneno yanashindwa, muziki huongea. Muziki huzungumza kwa hisia. Muziki huleta uwiano kati ya roho, nafsi na mwili.
Muziki ni mwanga wa mbalamwezi katika usiku wa kiza wa maisha. Muziki una nguvu ya uponyaji. Muziki unaweza kuponya majeraha ambayo dawa haiwezi kugusa.
Muziki hupunguza kiwango cha maumivu, wasiwasi na unyogovu. Ukiwa peke yako huna wa kukufariji, jaribu kusikiliza nyimbo za kuabudu. Muziki utakusaidia kuanza siku yako vizuri zaidi.
Muziki utakusaidia kulala vizuri. Muziki huboresha hisia wakati wa kuendesha gari. Muziki huongeza ubunifu.
Nyimbo za mapenzi huongeza uhusiano wa kimapenzi. Muziki wa chinichini utakusaidia kula kidogo na kufurahia chakula chako zaidi.
Muziki huongeza nguvu katika mazoezi. Watu huweza kukimbia parefu au kufanya mazoezi zaidi kwenye gym ikiwa wanacheza muziki.
Kwa mujibu wa Biblia. Nyimbo za kuabudu huinua roho zetu. Biblia inatuambia tusemezane sisi kwa sisi kwa zaburi, nyimbo, na Tenzi za Rohoni - na kuimba na kufanya muziki kutoka mioyoni mwetu kwa Bwana (Efe 5:9 & Kol 3:16).
Wimbo gani unaoupenda zaidi? Mie napenda sana wimbo wa TUFANI INAPOVUMA.
Ubarikiwe.