"Kwa maoni yangu, hili ni jambo jema, Rais kufungua kitegauchumi kikubwa hivi pwani ya Bagamoyo ni jambo la kheri.
Tufike mahali tujisikie proud wazawa sasa nao wanamiliki hoteli ya kiwango hicho. Ni hoteli chache sana pwani ya Bagamoyo zinamilikiwa na Wabongo.
Labda kama angefungua moja ya Sheraton, Holiday Inn, Marriott Marquez or Inter Continental labda watu wasingeshaa, wangeona its ok rais kufungua, lakini ikiwa ni hoteli ya Mbongo, ni maneno!.
JK amefanya jambo zuri katika promotion ya uwekezaji wa ndani, na sasa mahotelini humo, tukale wenyewe na kulala wenyewe, sio kungoja wazungu tuu.
Pamoja na umasikini wa Watanzania, wengi wa wapiga kilaji wazuri, ni sisi wenyewe. Mtu anakunywa 20,000-50,000 kwa siku akiwa na marafiki na kimwana, ila kuitoa family yake kwenda kushinda beach, or eating out ni issue!.:"
***************************
PASCO: Umeenda nje ya hoja. Mwanzilishi wa thread hakusema ni vibaya kwa JK kufungua hotel au kitega uchumi chochote, bali alikuwa analalmikia ile "cost" kwa umma katika ufunguzi huo. Settting ya tukio ilikuwa very elaborate.