SoC02 Nguvu ya Sayansi, Teknolojia na Jamii ya sasa

SoC02 Nguvu ya Sayansi, Teknolojia na Jamii ya sasa

Stories of Change - 2022 Competition

hanayna

Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
5
Reaction score
1
UTANGULIZI: 🔖Hivi sasa dunia 🌎imeangaza na kutumia teknolojia mbalimbali katika nyanja tofautitofauti ili kuweza kurahisisha mambo mbalimbali kidijitali💻, teknolojia sasa inafanya watu kujipatia kipato, ujuzi na vumbuzi mbalimbali kutokea kwa kundi la watu au mtu binafsi duniani kiujumla zamani watu walitumia baiskeli🚲kama chombo pekee cha usafiri ila sasa kuna usafiri wa aina mbalimbali kama ndege✈️,magari🚘, pikipiki🛵, treni🚊, meli🛳 na boti🚤 kupitia sayansi na teknolojia kuna vumbuzi mbalimbali zinazoendelea mfano utengenezaji wa magari yanayotumia gesi , treni za umeme hii husaidia kutochafuka kwa hali ya hewa.

Tanzania tumeona mtangazaji na mbunifu Masoud Ally Kipanya(kp)katengeneza gari linalotumia umeme hii imeonyesha ni jinsi gani sayansi na teknolojia inanguvu kiasi gani, watu wengi sasa duniani ni wanufaika wa teknolojia hususani vijana wameweza kuvumbua vitu mbalimbali mfano wao ni Maxence Melo: ni Mtanzania mwanzilishi wa Jamiiforums alivumbua mtandao wa jamii forums mnamo mwaka 2006 ukifahamika kama Jambo forums.

Evan Spiegel: mzaliwa wa Los Angeles California Marekani alivumbua mtandao wa snapchat ambao unarumika na watu wengi duniani aliacha chuo na kuweza kuendeleza mtandao huo bila kujali chochote kitakachotokea mbeleni alizindua snapchat mnamo mwaka 2011.

Mark Zuckerberg;
mvumbuzi wa mtandao wa facebook aliyezaliwa 4/5/1984 nchini Israel alivumbua mtandao huo wa kijamii akiwa bado mwanafunzi wa chuo kikuu cha Havard na kuanzisha Facebook rasmi mwaka 2004


VIPI JAMII INAWEZA NUFAIKA KUPITIA SAYANSI NA TEKNOLOJIA/MITANDAO YA KIJAMII?

1. Kuuza, kununua au kupata huduma katika mitandao ya kijamii mbalimbali au tovuti mfano wa tovuti ni Alibaba, Kikuu na Amazon mitandao ya kijamii ni kama instagram, whatsApp na facebook.

2. Kujuana na watu mbalimbali duniani kubadilishana mawazo kupata mitazamo chanya itakayomsaidia mtu kupiga hatua mbele, kupeana ujuzi au fursa mbalimbali kama ujuzi juu ya biashara ya forex au biashara mtandao(business networking).

3. Kupata burudani mbalimbali kwa mda uupendao kupitia youtube, instagram, jamii forums au tiktok watu wengi hutumia mitandao ya kijamii kwa mahitaji yao ila vijana wengi wanapenda mitandao ya kijamii kwa dhumuni au malengo mbalimbali ikiwemo burudani au michezo

4. Kupata elimu na ujuzi mbalimbali kupitia vitu tofautitofauti vya kiteknolojia mfano kupata elimu au ujuzi wa mapishi, sayansi ya kompyuta, ubunifu wa mitindo kama nguo au nywele na mapambo.

5. Teknolojia imesaidia kuunda vifaa mbalimbali kama vifaa vya hospitali, shule, vifaa vya kielekroniki kama redio, runinga, kompyuta pia magari

6. Teknolojia imesaidia kurahisisha usafiri mbalimbali kama vile baiskeli,magari,pikipiki,meli,treni na ndege.

7. Kupata taarifa mbalimbali ambazo mtu hana uhakika nazo kupitia google , firefox na googlechrome.

ATHARI ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIA/MITANDAO YA KIJAMII

1. Inapelekea uraibu (kutumia mitandao ya kijamii kupitiliza)kwa watu hususani vijana wa umri wa bareghe wengi wao hushinda katika mitandao ya kijamii kufanya vitu visivyokuwa na faida kwao unakuta kijana anatumia fedha nyingi kununua vifurushi (bundles) kwa malengo ya kupeluzi mtandaoni.

2. Inapelekea kijana kutoendelea kijamii, kisaikolojia na kiuchumi mfano mtu anamiliki simu yenye bei kubwa kama iphone, samsung, nokia, au infinix na anasema hana mtaji wakati mtaji ni ile simu yake.

3. Mitandao ya kijamii inapelekea upotofu wa maadili na nidhamu kwa watu wengi hususani vijana wanaiga vutu mbalimbali ambavyo havina manufaa kwao.

4. Inapelekea maafa na uharibifu wa vitu mfano tumeona katika vita vya ukraini na Urusi uwepo wa teknolojia imepelekea kuteneneza mabomu/makombora ambayo yameweza kuleta maafa makubwa na uharibifu wa vitu vingi.

5. Inapelekea ukosefu wa ajira kwa nguvu kazi ya kijana hivi sasa vitu vingi hutumia teknolojia ya mashine mbalimbali na kompyuta ili kurahisisha kazi nyingi katika sekta mbalimbali.

6. Inapelekea kuibuka/kukuza uharifu wa mitandaoni, uwepo wa teknolojia ya komputa kuna wadukuzi /wezi katika mitandao upekua taarifa za mtu binafsi na kuiba au kufungia akaunti za watu pua uibaji wa data au vitu vya faragha.

7. Inapelekea athari kwa afya ya binadamu, sayansi na teknolojia imeweza kuleta vitu vingi ambavyo vimekuwa ni faida kwa binadamu ila pia huleta hasara mfano television inapelekea uharibifu wa macho.

JE! Ni VIPI JAMII YA SASA / KIJANA ANAWEZA KUCHANGAMKIA FURSA KUPITIA SAYANSI NA TEKNOLOJIA?

1.
kupitia katika mitandao ya kijamii mbalimbali kama youtube, jamii forums, facebook na instagram kuna video au mafunzo(tutorials) mbalimbali zitakazo muwezesha mtu kupata ujuzi juu ya kitu fulani mfano upishi, utengenezaji wa bidhaa tofautitofauti, urembo na mitindo.

2. Kujifunza kuhusiana na mifumo mbalimbali kama(tehama) ili kupata ujuzi utakao mwezesha kuunda mifumo itakayoweza kutumika katika sekta za Afya,mifumo ya fedha, mitandao ya kijamii na tovuti mbalimbali.

3.kufanya biashara kupitia tovuti (website) au mitandao ya kijamii ,biashara mtandao (e-business) haina gharama sana kwa mfano ulipaji kodi wa pango la boashara, pia inasaidia bidhaa inapatwa kuonwa na watu wengi kwa mda mchache duniani(worldwide).

4. Kushiriki au kutembelea katika maonyesho yanayofanyika katika eneo fulani yanayohusiana na sayansi nateknolojia ili kupata ujuzi au kuonyesha ujuzi na kujifunza vitu tofautitofauti.


VIPI SERIKALI INAWEZA KUSAIDIA KUKUA KWA SAYANSI NA TEKNOLOJIA?
1. Kuwapa elimu wananchi juu ya uwepo wa teknolojia mbalimbali mfano kilimo utumiaji wa treka, mbegu bora na utumiaji wa mbolea katika mazao hii husaidia kukua haraka kwa mazao pia kutumia/kupulizia madawa kwenye mazao ili kuua vijidudu.

2. Kuwapa hamasa/ kuwafunza wanafunzi mashuleni juu ya sayansi na teknolojia mbalimbali zilizopo duniani na vumbuzi zinazofanyika ili wapate hamasa juu ya teknolojia.

3. Kuunda vikundi mbalimbali vitakavyowezesha watu kupata mafunzo juu ya sayansi na teknolojia ambazo zitaweza kuwa tija na kuleta manufaa.

HITIMISHO: Ulimwengu wa sasa umebwebwa na sayansi na teknolojia kwa dhumuni la kurahisisha vitu pia imetusaidia karika nyanja mbalimbali kama kurekebisha miundombinu, kuunda mifumo ya mawasiliano, kuleta ajira kwa watu, watu kuvumbua vipajia vyao pia na kurahisisha vitu vingi katika dunia. Hivyo sisi kama jamii ya kisasa tunapaswa kuchangamkia fursa mbalimbali zitokanazo na sayansi na teknolojia ili kuua mbele kiuchumi.

Ahsantee kwa kusoma🙏
 
Upvote 3
Back
Top Bottom