Gabeji
JF-Expert Member
- Sep 10, 2024
- 1,530
- 1,903
Bila shaka wote ni wazima wa afya njema. Kudai katiba mpya kwa CCM au wanasiasa ni sawa na kudai uhuru kutoka kwa "mkoloni" kwa sababu ya ubinafsi (egoism). Katiba ndio injini ya nchi yoyote ile duniani.
Watanzania ni kama mgonjwa wa akili tu! Ambaye anamini kuwa katiba mpya italetwa na CCM au wanasiasa. Hakuna raisi atakubali kirahisi kupunguziwa madaraka, utukufu, hadhi, nguvu, mamlaka, n.k. Huyo mtu hayupo duniani, hata mbinguni. Bila shaka atakuwa chizi. Hata Mungu alipotaka kupunguziwa madaraka na shetani, Mungu alimfukuza shetani kabisa katika himaya yake, kwa mujibu wa hadithi za Wakristo.
Madaraka ni matamu mno, tena mno; kupewa utukufu ni kuzuri mno kwa binadamu mwenye akili timamu. Hivyo basi ni "nguvu ya umma" pekee ambayo inaweza kuleta katiba mpya. Baada ya miaka 15 ijayo, ninaamini Watanzania wengi watakuwa wameelimika juu ya umuhimu wa katiba mpya.
Baada ya miaka hiyo pia, Watanzania watakuwa wamechoka kusikia familia zile zile nenda rudi, miaka yote wakiwa ni viongozi, koo zao, ndugu zao, watoto wao, wajukuu wao, makabila yao, dini zao, kanda zao. Ndipo sasa Watanzania wote bila kujali dini, wala itikadi, wala kabila wataungana kwa pamoja na kudai katiba mpya. "Hakuna masika yasiyo kuwa na ncha." Mungu ibariki Tanzania.
— Mwinjilist wenu Gabeji.